Afisa Utumishi wa
Mahakama Kuu, Bwana Faridi Mnyamike (Aliyesimama) akitoa mafunzo ya namna ya
uandaaji taarifa na nakala za hukumu.
Na
Amina Ahmad, Mahakama Kuu-Tanga
Uongozi wa Mahakama
Kanda ya Tanga uliendesha mafunzo elekezi kwa Mahakimu,Watendaji na watumishi
wanaoshughulika na uandaaji, uchakataji na uwasilishaji wa takwimu za mashauri
ikiwa ni utekelezaji wa nguzo ya pili (2) ya mpango mkakati wa Mahakama.
Miongoni mwa mada
zilizotolewa ni pamoja na usafishaji wa mashauri kwenye mfumo wa JSDS II (Data
cleanup), ufanikishaji wa utoaji na usambazaji wa nakala za hukumu kwa wadau na
posta hadi mlangoni na ujazwaji wa fomu mbalimbali za takwimu za kimashauri zinazoandaliwa kila
mwezi, robo mwaka na mwisho wa mwaka.
Sambamba na mafunzo
hayo, Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu, Mhe. Amiri Mruma alizindua barua pepe ya
wadau wa takwimu za mashauri (statistics
tangazone group mail) ambayo itasaidia/kurahisisha usimamizi na uthibiti wa
mienendo ya uandaaji na utumaji wa takwimu kwa usahihi na kwa wakati.
Katika kikao hicho, jumla ya maazimio kumi na tisa (19) yaliafikiwa yanayolenga kuleta utendaji shirikishi na matokeo chanya katika Nyanja za utendaji wa kila siku wa shughuli za kimahakama na uendeshaji.
Jaji
Mfawidhi wa Mahakama Kuu, Mhe. Amiri Mruma (aliyesimama) akizungumza na wadau
waliohudhuria mafunzo. Kushoto kwake ni Naibu Msajili Mhe. Francis Kabwe na
kulia kwake ni Mtendaji wa Mahakama, Ndugu Ahmed Selemani Ng’eni.
![]() |
Hakimu Mkazi Mfawidhi
wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Tanga, Mhe. Desdery Kamugisha akitoa mafunzo ya
namna bora ya uandaaji wa takwimu za mashauri.
|
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni