Jaji
Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Hamis Juma ametaka ushirikiano mzuri uliopobaina ya Mahakama ya Tanzania na Benki ya Dunia kuendelezwa.
Ameyasema
hayo leo alipotembelewa na Timu ya Wataalamu kutoka Benki ya Dunia waliopo
nchini kwa ajili ya ufuatiliaji wa shughuli mbalimbali zinazotekelezwa kwa
ushirikiano na Benki hiyo.
“Tunashukuru
kwa namna ambavyo tumeweza kushirikiana kwa kiasi ambacho sasa tunaweza kuona
mabadiliko, mathalani kupungua kwa malalamiko kutoka kwa wafungwa Magerezani”,
amesema Jaji Mkuu.
Naye
Mtendaji Mkuu wa Mahakama Bw. Hussein Kattanga amebainisha kuwa mradi wa
maboresho unaotekelezwa na Mahakama ni wa aina yake kwa kuwa unahusu mabadiliko
ya watu. Mbali ya kushukuru kwa
ushirikiano, amesisitiza kuwa Mahakama inafanya jitihada mbalimbali kutekeleza
mipango yake kwa kuchukua mifano bora kutoka nchi za Ufaransa na Kazakhstan.
Kwa
upande wake Bw. Waleed Malik ameonyesha kuridhishwa kwake na kiwango cha
maboresho kilichofikiwa katika Mahakama.
“Nimeridhishwa na kiwango na ubora wa huduma
zinazotolewa kwenye maonesho na utoaji elimu kwa ujumla kule Dodoma. Nimefurahia uratibu mzuri wa maadhimisho ya
wiki ya sheria”, amesema Bw. Malik. Ameongeza
kuwa ameweza kubaini matokeo chanya na yanayoonekana.
Ujumbe
wa Benki ya Dunia unaongozwa na Bi. Deborah Isser. Wengine ni Bw. Waleed Malik na Bi. Clara
Meghani. Katika ziara hiyo ujumbe huo utatembelea kanda za Mbeya, Mwanza, Mara
na pia Chuo cha Uongozi wa Mahakama, Lushoto.
Aidha, kikao hicho
kilihudhuriwa pia na Jaji Kiongozi Mhe. Dkt. Eliezer Feleshi; Msajili Mkuu wa
Mahakama Mhe. Katarina Revocati; Mkuu wa Timu ya Maboresho ya Mahakama Bw.
Solanus Nyimbi na Mkuu wa Kitengo cha Maboresho cha Mahakama Mhe. Zahra Maruma.
Jaji Mkuu wa Tanzania,Mhe. Profesa Ibrahim Hamis Juma (kushoto) akisalimiana na ni Mjumbe kutoka Benki Deborah Isser baada ya kumtembelea ofisini, iliyoko Mahakama ya Rufaa jijini Dar es Salaam. |
Jaji Mkuu wa Tanzania,Mhe. Profesa Ibrahim Hamis Juma akizungumza na wajumbe kutoka Benki ya Dunia baada ya kumtembelea ofisini , iliyoko Mahakama ya Rufaa jijini Dar es Salaam
Mjumbe
kutoka Benki ya Dunia , Deborah Isser (wa kwanza kulia)akizungumza
jambo wakati ujumbe kutoka Benki ya hiyo ulipotembelea ofisi ya Jaji Mkuu, iliyopo Mahakama ya Rufaa. |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni