Jaji Kiongozi, Mahakama
Kuu ya Tanzania, Mhe. Jaji Dkt. Eliezer Mbuki Feleshi amewasili Mkoani Mbeya
Aprili 08, 2019 kuanza rasmi ziara ya kikazi katika Mahakama Kanda ya Mbeya.
Katika ziara yake ya
siku mbili (2) ndani ya Kanda hiyo, Mhe. Jaji Kiongozi, anatarajiwa kukagua
miradi mbalimbali ya ujenzi wa Mahakama inayoendelea pamoja na kuzungumza na
Watumishi.
Lengo la ziara ni
kujua hali ya maendeleo ya utekelezaji
wa maboresho ya huduma mbalimbali za
Mahakama na vilevile kuwakumbusha Watumishi wa Mhimili huu kuendelea
kutekeleza jukumu la msingi la utoaji haki nchini kwa ubora wa hali ya juu kwa manufaa
ya wananchi.
Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Jaji Robert Makaramba (kushoto) akimlaki Mhe. Jaji Kiongozi pindi alipowasili mkoani Mbeya kwa ziara ya kikazi.
Mhe. Jaji Kiongozi akiendelea kusalimiana na baadhi ya Viongozi wa Mahakama Kanda ya Mbeya waliofika kumlaki. Anayesalimiana nae ni Naibu Msajili Mfawidhi wa Mahakama Kuu-Kanda ya Mbeya, Mhe. George Herbert na wa kwanza kushoto ni Naibu Msajili, Mahakama Kuu, Kanda ya Mbeya, Mhe. William Mutaki.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni