Balozi wa Uholanzi
nchini Tanzania Mhe. Jeroen Verneul amesema uholanzi iko tayari kuisaidia
Mahakama ya Tanzania katika nyanja za uwezeshaji kitaaluma ili haki iweze
kupatikana kwa wakati na tayari imetenga fedha kwa ajili hiyo.
Balozi Verneul alisema
hayo hivi karibuni alipofika ofisini kwa Jaji Mkuu kwa ajili ya kujitambulisha
na kubadilishana mawazo na Kiongozi huyo wa Mhimili wa Mahakama.
Awali akielezea mikakati
ya Mahakama, Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma alisema hivi
sasa Mahakama inajipanga kuona uwezekano wa kuihuisha sheria ya Usuluhishi (Arbitration
Act) na ile ya Kimataifa ili iwe na wigo mpana na rahisi katika Mahakama zetu.
“Hii itasaidia sana
wakati Serikali yetu inaingia katika uchumi wa viwanda na kuwa na wawekezaji wasiokuwa na mashaka juu ya
uwekezaji wao endapo mifumo ya
usuluhishi wa migogoro ya kibiashara ina
utaratibu mzuri”, alisema Jaji Mkuu.
Alisema katika bara la
Afrika zipo nchi zimefanya hivyo na sasa zina mafanikio makubwa katika utatuzi
wa migogoro ya wawekezaji, hivyo yuko tayari kutumia vyombo vyote vinavyohusika
kuona endapo sasa sheria iliyopo inahuishwa ili kuendana na matakwa ya karne
hii.
Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akisalimiana na Balozi wa Uholanzi nchini Tanzania Mhe. Jeroen Verneul alipomtembelea ofisini kwake jijini Dar es salaam.
Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akimkabidhi Balozi wa Uholanzi nchini Mhe Jeroen Verneul kitabu cha Mpango Mkakati wa miaka mitano wa Mahakama ya Tanzania.
Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma pamoja na Balozi wa Uholanzi nchini Mhe Jeroen Verneul wakibadilishana mawazo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni