Na
Magreth Kinabo
Jaji Mkuu wa
Mahakama ya Tanzania, Mhe. Profesa Ibrahim Juma amesema Mahakama ya Tanzania
iko tayari kushirikiana na Taasisi ya Kimataifa ya Upatanishi ‘International
Chamber of Commerce’ (ICC) ili kuwezesha Mahakama kusikiliza migogoro kwa njia
ya mfumo wa upatanishi( Abitration).
Kauli hiyo
imetolewa leo na Jaji Mkuu, ofisini
kwake jijini Dar es Salaam ,wakati
alipofanya mazungumzo na ujumbe watu watano kutoka taasisi hiyo, uliongozwa na
Makamu wa Rais wa taasisi hiyo, Profesa . Dkt.
Mohamed Wahab.
Awali Makamu
huyo wa taasisi hiyo alisema wamefika hapa nchini ili kufanya mazungumzo na
Jaji Mkuu, Profesa Juma kuhusu kushirikiana na Mahakama ya Tanzania kuiwezesha kusikiliza migogoro kwa njia ya mfumo wa
upatanishi.
Profesa, Dkt.
Wahab aliongeza kwamba tayari nchi nyingine zimeruhusu Mahakama, kutumia mfumo huo wa upatanishi na umeonyesha kufanikiwa, ambapo alitolea mfano nchi ya
Afrika Kusini na Mauritania, hivyo wangependa kuona na Tanzania inautumia na taasisi hiyo itatoa mafunzo kwa majaji.
“Ni tunaiomba Tanzania kutengeneza kanuni ili
kuwezesha mfumo huo wa upatanishi
kuweza kufanya kazi katika Mahakama za Tanzania,'' alisema Profesa.Dkt. Wahab.
Jaji Mkuu
alisema yuko tayari kuwezesha mfumo huo kuanza kutumika nchini kwa kuwa ni muhimu
na utawezesha migororo
kusikilizwa haraka.
“Tuna Sheria ya Upatanishi, ni sheria ya zamani
hivyo kuna haja ya kuihuisha ili iendane na mahitaji ya sasa,” alisema Profesa
Juma.
Alisema
Mahakama inatumia njia ya upatanishi
ndani ya kesi za madai, lakini haujaweza kufanya kazi vizuri kwa sababu
ya kutoeleweka ipasavyo miongoni mwa wadaawa.
Hivyo aliongeza
kwamba ni vizuri majaji na mawakili wakapatiwa mafunzo juu ya masuala
hayo.
Profesa Juma
aliutaka ujumbe huo kuandaa andiko na kuhusu mfumo huo na kuonyesha mapendekezo
yao.
Ujumbe huo umekuwepo
nchini tangu Julai 17 na Julai 19 ,
mwaka huu na umefanya mazungumza na ujumbe wa Tanzania kuhusu masuala ya upatanishi ndani na nje ya nchi , ikiwemo Siku
ya Upatanishi iliyofanyika kwenye hoteli ya Slipway, Dar es Salaam Julai
18,mwaka huu na utakuja tena mwakani,
Jaji Mkuu wa Mahakama
ya Tanzania, Mhe. Profesa Ibrahim Juma,(katikati) akiwa na ujumbe wa watu watano kutoka Taasisi
ya Kimataifa ya Upatanishi (ICC), ukiongozwa na Makamu Rais wa ICC, kwanza
kushoto Profesa . Dkt. Mohamed Wahab anayesaini katika kitabu cha
wageni.
Makamu wa Rais wa Taasisi
ya Kimataifa ya Upatanishi(ICC) wa kwanza kushoto Profesa . Dkt.
Mohamed Wahab(aliyenyoosha mikono) akizungumza jambo na Jaji Mkuu wa
Tanzania, Profesa Ibrahim Juma mara baada ya kumtembelea Ofisini kwake, akiwa
na wajumbe wengine wa ICC.
Jaji Mkuu wa Mahakama
ya Tanzania, Mhe. Profesa Ibrahim Juma,(katikati) akizungumza na ujumbe wa watu watano kutoka Taasisi
ya Kimataifa ya Upatanishi (ICC).
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni