Na
Magreth Kinabo.
Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania,
Mhe. Dkt. Eliezer Feleshi amewataka wananchi kuwa na mwamko wa kutembelea Banda
la Maonesho la Mahakama ya Tanzania ili kujifunza shughuli mbalimbali zinazofanywa
na mahakama, wakiwemo wadau wake.
Akizungumza alipotembelea
banda hilo jana kwenye Maonesho
ya 43 ya Biashara ya Kimataifa , Jaji Kiongozi alisema Mahakama ya Tanzania
imeboresha huduma mbalimbali ikiwemo mfumo wa kusajili na kutafuta kesi kwa
kutumia mfumo wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano(TEHAMA), pamoja na mfumo wa kuwatambua mawakili feki na halali.
“Wananchi wajitahidi kujitokeza kwa
wingi katika Banda la Mahakama ya Tanzania, Kwa kuwa ni fursa ya kuweza kufahamu
mambo, ambayo waliyokuwa hawayafahamu,” alisema Jaji Kiongozi.
Akizungumzia kuhusu mlundikano wa kesi
mahakamani alisema kwa sasa kuna maboresho yanayoendelea kufanyika hatua iliyosababisha
kutokuwepo kwa mlundikano wa kesi mahakamani.
Jaji Kiongozi aliongeza kwamba katika
maonesho hayo Mahakama imekuwa ikipokea maoni mbalimbali kutoka kwa wananchi,
ambayo itayatathimini na kuyafanyia kazi
kwa lengo la kuboresha huduma zake.
Akifafanua kuhusu Mahakama inayotembea
(Mobile Court) alisema, itaanza kufanya kazi hivi karibuni katika jiji la Dar es Salaam na Mwanza na kuongeza ongeza
kwamba Mahakama inayotembea itakuwa
ikisikiliza kesi ambazo si za muda mrefu na zisizo na mashahidi wengi ili kutoa
haki kwa wakati.
Baada ya kutembelea banda la Mahakama,
Jaji Kiongozi Mhe. Dkt. Feleshi pia alitembelea mabanda ya taasisi nyingine za
Serikali ili kujionea shughuli nyingine za kimaendeleo zinazofanywa na taasisi
hizo.
Miongoni mwa mabanda hayo ni banda la
Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Polisi, Uhamiaji, Wizara ya Maliasili Utalii na
Magereza.
Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania,
Mhe. Dkt. Eliezer Feleshi akitia saini kwenye kitabu cha wageni mara baada ya
kuwasili katika Maonesho ya 43 ya Biashara ya Kimataifa kwenye Ofisi za Mamlaka
ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE). Kushoto ni Naibu Mkurugenzi Mkuu
wa TANTRADE, Bi. Latifa Khamis.
Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya
Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE), Bi Latifa Khamis (Kushoto) akimuonesha
Jaji Kiongozi Mhe. Dkt. Eliezer Feleshi ratiba ya matembezi ya Maonesho ya 43 ya
Biashara ya Kimataifa
yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Julius.K
Nyerere vilivyopo jijini Dar es Salaam, Kulia ni Naibu Msajili Mahakama Kuu
Masjala Kuu Mhe. Sharmillah Sarwatt.
Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya
Tanzania Mhe Dkt. Eliezer Feleshi akipokea maelezo
jinsi Mfumo wa kusajili kesi mtandaoni unavyofanya kazi. Anaetoa maelezo hayo
(kushoto) ni Afisa Tehama wa Mahakama Kuu ya Tanzania Bw. Athumani Kanyegezi.
Jaji Kiongozi wa Mhakama Kuu ya Tanzania
Mhe. Dkt. Eliezer Feleshi akitoa maelezo kwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka
ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) Bi. Latifa Khamis jinsi Mfumo wa
kusajili kesi kwa njia ya kielektroniki unavyofanya kazi.
Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya
Tanzania Mhe.Dkt Eliezer Feleshi akipokea maelezo kutoka kwa Afisa Mkutubi wa
Mahakama ya Tanzania Bw. Salum Tawan alipotembelea maonesho ya 43 ya Biashara
yanayoendelea jijini Dar es Salaam.
Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe.Dkt. Eliezer Feleshi akiondoka katika banda la Mahakama ya Tanzania mara baada ya kutembelea banda hilo lililopo katika Maonesho ya 43 Biashara ya Kimataifa (SABASABA). Kulia ni Naibu Msajili Mahakama Kuu Masjala Kuu Mhe. Sharmillah Sarwatt na kushoto ni Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam Mhe. Joseph Fovo.
(Picha na Dennis Buyekwa).
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni