Alhamisi, 11 Julai 2019

JENGO LA MAHAKAMA KUU KIGOMA LAKAGULIWA

 Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Mhe. Katarina Revocati akizungumza na baadhi ya wajumbe wa Menejimenti ya Mahakama ya Tanzania mara ya baada ya kufanya ukaguzi kwenye jengo jipya la Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Kigoma. Wajumbe hao wametembelea jengo hilo kwa ajili ya kukagua likiwa katika hatua za mwisho za ukamilishwaji wake. Aidha, Msajili Mkuu amewapongeza Mkandarasi pamoja na Mshauri Mwelekezi kwa kufanya kazi nzuri na kumaliza kwa wakati.

 Mtendaji wa Mahakama ya Rufani Bwn. Solanus Nyimbi akisisitiza jambo alipokuwa akizungumza na baadhi ya wajumbe wa Menejimenti ya Mahakama mara baada ya kukagua jengo jipya la Mahakama Kuu Kigoma.

  Jengo la Mahakama Kuu ya Tanzania kanda ya Kigoma linavyoonekana kwa mbele  likiwa katika hatua za mwisho za ukamilishwaji wake.


 Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Mhe. Katarina Revocati (mbele katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wajumbe wa Menejimenti ya Mahakama ya Tanzania mara ya baada ya kufanya ukaguzi kwenye jengo jipya la Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Kigoma. Wa pili Kushoto ni Mtendaji wa Mahakama ya Rufani Bwn. Solanus Nyimbi na wa pili kulia ni Mtendaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Bwn. Leonard Magacha.  
Wajumbe wa Menejimenti ya Mahakama ya Tanzania pia walitembelea na kukagua jengo litakalotumika kama nyumba ya Majaji likiwa katika hatua za kati za ujenzi wake. Mahakama inajenga nyumba mbili kwa ajili ya Majaji mkoani Kigoma.
Wajumbe wakiwa juu ya jengo hilo wakiendelea na ukaguzi

Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Mhe. Katarina Revocati akionyesha jambo wakati wajumbe wa Menejimenti ya Mahakama ya Tanzania wakikagua  jengo jipya la Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Kigoma.


Jengo linavyoonekana kwa ndani katika gorofa ya tatu. 
Mandhari inavyoonekana kwa nje ya jengo hilo.  

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni