Pichani ni muonekano wa
jengo jipya la Mahakama ya Wilaya Chato lililopo mkoani Geita, jengo hilo la
kisasa lipo katika hatua za mwisho za ukamilishwaji wake kabla ya kuanza kutumika rasmi.
Msajili Mkuu- Mahakama
ya Tanzania, Mhe. Katarina Revocati (wa kwanza kushoto), Mtendaji wa Mahakama ya
Rufani (T), Bw. Sollanus Nyimbi (mbele kulia) pamoja na sehemu ya Wajumbe wa
Menejimenti ya Mahakama ya Tanzania na Watumishi wa Mahakama ya Wilaya Chato
wakiwa eneo la jengo hilo jipya tayari kwa ukaguzi. Lengo la
ukaguzi ni kuhakikisha kuwa kila kitu kimekaa sawa kabla ya kuzinduliwa na kuanza kutumika
rasmi kwa jengo hilo. Ukaguzi huo umefanyika mapema Julai 13, 2019.
Ukaguzi wa jengo
ukiendelea katika sehemu mbalimbali za jengo hilo.
Msajili Mkuu- Mahakama
ya Tanzania, Mhe. Katarina Revocati (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi
na Watumishi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Geita na Mahakama ya Wilaya Chato
iliyopo mkoani Geita.
Picha ya pamoja,
Watumishi wa Mahakama mkoani Geita pamoja na sehemu ya Wajumbe wa Menejimenti
ya Mahakama ya Tanzania walipotembelea eneo hilo kwa ajili ya ukaguzi wa
majengo mapya ( Mahakama ya Wilaya Chato na Mahakama ya Hakimu Mkazi- Geita)
Muonekano wa jengo
jipya la Mahakama ya Hakimu Mkazi Geita lililopo katika hatua za mwisho za
ukamilishwaji wake, jengo hili pia limekaguliwa na Wajumbe wa Menejimenti ya
Mahakama.
Sehemu ya Maafisa Wakuu
wa Mahakama ya Tanzania wakiwa katika jengo jipya la Mahakama ya Hakimu Mkazi
Geita tayari kwa ukaguzi.
Mkurugenzi wa
Rasilimali Watu na Utawala, Mahakama ya Tanzania, Bw. Edward Nkembo
(aliyenyoosha kidole) akiwaonyesha kitu baadhi ya Wajumbe wa Menejimenti ya
Mahakama pindi walipokuwa wakikagua jengo la Mahakama ya Hakimu Mkazi Geita.
Mhandisi kutoka Kampuni
ya MOLADI Tanzania ( Kampuni iliyojenga majengo ya Mahakama ya Mahakama ya
Hakimu Mkazi Geita na Mahakama ya Wilaya Chato) , Bw. Noel akieleza jambo kwa
Wajumbe kuhusiana na jengo hilo ambapo kwa mujibu wake jengo hilo tayari
limekamilika kwa asilimia kubwa na sasa wanaendelea kufanya marekebisho madogomadogo
katika baadhi ya sehemu za jengo hilo.
Muonekano wa jengo la
sasa linalotumika kwa shughuli za Mahakama ya Hakimu Mkazi/Mkoa Geita,
upatikanaji wa majengo mapya ya Mahakama katika mkoa huu utawezesha huduma ya
utoaji haki kupatikana katika mazingira bora na rafiki zaidi kwa manufaa ya
wananchi. Moja ya malengo ya Mahakama ya Tanzania ni pamoja na kuboresha na
kujenga miundombinu ya majengo rafiki kwa manufaa ya utoaji wa huduma ya haki
kwa wananchi.
(Picha na Mary
Gwera-Mahakama, Geita)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni