Sehemu ya Wajumbe wa
Menejimenti ya Mahakama ya Tanzania wakiingia katika jengo jipya la Mahakama
Kuu Kanda ya Musoma kwa lengo la kulikagua kufuatia kukamilika kwa asilimia
kubwa ya ujenzi wake. Ukaguzi umefanyika Julai 12, 2019.
Upatikanaji wa huduma ya Mahakama Kuu mkoani Mara utawarahisishia wananchi wa mkoa huu kuondokana na aza ya kusafiri kufuata huduma ya Mahakama Kuu- Kanda ya Mwanza kama ambavyo ilikuwa ikifanyika hapo awali.
Katika ziara hiyo, Wajumbe hao wametembelea Ofisi ya muda ya Jaji Mfawidhi- Mahakama Kuu, Kanda ya Musoma, wamekagua pia ujenzi wa nyumba mbili za Majaji wa Kanda hiyo.
Katika ziara hiyo, Wajumbe hao wametembelea Ofisi ya muda ya Jaji Mfawidhi- Mahakama Kuu, Kanda ya Musoma, wamekagua pia ujenzi wa nyumba mbili za Majaji wa Kanda hiyo.
Muonekano wa jengo la
Mahakama Kuu Musoma linavyoonekana kutokea nje ya uzio.
Ukaguzi ukiendelea sehemu mbalimbali za jengo hilo.
Mkandarasi kutoka DF Mistry Company Ltd waliojenga jengo la Mahakama Kuu akiwasilisha kwa wajumbe wa Menejimenti pamoja na sehemu ya Watumishi wa Mahakama Musoma hatua mbalimbali walizopitia katika ujenzi wa jengo hilo lililoanza kujengwa 2017. Wa kwanza kulia ni Mtendaji Mkuu, Mahakama ya Tanzania, Mhe. Hussein Kattanga, kulia kwake ni Msajili Mkuu, Mahakama ya Tanzania, Mhe. Katarina Revocati.
Picha ya pamoja mbele ya jengo jipya la Mahakama Kuu-Kanda ya Musoma.
(Picha na Mary Gwera, Mahakama-Musoma)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni