Jaji Mkuu wa Tanzania,
Mhe.Prof. Ibrahim Hamis Juma akimkabidhi nyenzo za kazi ‘instruments’ kwa Mhe. Godfrey
Isaya za kuwa Hakimu Mkazi Mfawidhi, Mahakama ya Hakimu Mkazi-Kisutu. Hafla
fupi ya kukabidhiwa nyenzo za kazi pamoja na kuapishwa Mahakimu Wakazi
imefanyika katika Ukumbi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Arusha Desemba
03, 2019.
Jaji Mkuu wa Tanzania,
Mhe.Prof. Ibrahim Hamis Juma akimuapisha, Mhe. Upendo Moshi kuwa Hakimu Mkazi
wa Mahakama ya Mwanzo, Mhe. Moshi ni mmoja wa Mahakimu wapya walioajiriwa hivi
karibuni na Tume ya Utumishi wa Mahakama.
Jaji Mkuu wa Tanzania,
Mhe.Prof. Ibrahim Hamis Juma akimuapisha, Mhe. Veronica
Mwanasenga kuwa Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Mwanzo.
Jaji Mkuu wa Tanzania,
Mhe.Prof. Ibrahim Hamis Juma akimuapisha, Mhe. Oscar Kahyoza kuwa Hakimu wa
Mahakama ya Mwanzo Serengeti.
Jaji Kiongozi, Mahakama
Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt. Eliezer Mbuki Feleshi akimuapisha Mhe. Niku
Mwakatobe kuwa Naibu Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania, kabla ya kuteuliwa
kuwa Naibu Msajili, Mhe. Mwakatobe alikuwa Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya
Hakimu Mkazi-Arusha.
Pichani ni Naibu Msajili Mwandamizi, Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Messeka Chaba (aliyesimama), Mtendaji, Mahakama Kuu ya Tanzania, Bw. Leonard Magacha (aliyeketi- mwenye shati ya bluu bahari) na sehemu ya Watumishi wa
Mahakama waliohudhuria katika hafla hiyo fupi ya Uapisho.
Jaji Mkuu wa Tanzania,
Mhe.Prof. Ibrahim Hamis Juma akizungumza na Wahe. Mahakimu aliowaapisha.
Amewataka kuviishi viapo vyao na kujiepusha na vitendo vya rushwa na vilevile
kutoa haki kwa wananchi kwa wakati na bila upendeleo.
Mhe. Jaji Mkuu wa
Tanzania pamoja na baadhi ya Majaji na Watendaji wa Mahakama wakiwa katika picha
ya pamoja na Wahe. Walioapishwa na kukabidhiwa nyenzo za kazi.
Picha ya pamoja na baadhi
ya Majaji wa Mahakama ya Rufani walioshiriki katika hafla hiyo.
Picha ya pamoja na
baadhi ya Watendaji na Wasajili wa Mahakama.
(Picha na Mary Gwera, Mahakama-Arusha)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni