MATUKIO
KATIKA PICHA
Wahe. Majaji
wakifuatilia mada inayotolewa na Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma (hayupo pichani).
Jaji Mkuu wa Tanzania,
Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akitoa Mada kwa Wahe. Majaji katika mafunzo
elekezi yanayoendelea kutolewa kwa Wahe. Majaji Wafawidhi yanayofanyika katika
Ukumbi wa ‘EAC’ jijini Arusha.
Jaji Mfawidhi, Mahakama
Kuu-Kanda ya Dar es Salaam, Mhe Rhoda Beatrice Mutungi akitoa mada inayohusiana
na masuala ya Ukaguzi wa Mahakama kwa Wahe. Majaji Wafawidhi.
Mkuu wa Kitengo cha
Maboresho, Mahakama ya Tanzania, Mhe. Zahra Maruma akitoa mada kwa Wahe. Majaji
(hawapo pichani) juu ya Maendeleo ya utekelezaji wa Mpango Mkakati wa miaka
mitano (5) wa Mahakama (2015/2016-2019/2020), Maeneo ya kuongeza nguvu pamoja
na mipango ya baadae.
Wahe. Majaji
wakifuatilia mada inayotolewa.
Jaji Mfawidhi, Mahakama
Kuu-Divisheni ya Kazi, Mhe. Sophia Wambura akichangia jambo.
Jaji Mfawidhi, Mahakama
Kuu-Kanda ya Mbeya, Mhe. John Utamwa akichangia mada.
Jaji Mfawidhi wa
Mahakama Kuu-Kanda ya Musoma, Mhe. John Kahyoza akichangia jambo katika mafunzo
hayo.
Mmoja wa Wawezeshaji wa Mafunzo kutoka chuo cha ‘ESAMI’ Prof.
Dkt. Michael Munkumba akitoa mada kwa Wahe. Majaji Wafawidhi.
Afisa Tehama, Mahakama ya Tanzania, Bw. Othman Kanyegezi akitoa
mada kuhusu Mfumo wa kielektroniki
wa Usimamizi wa Mashauri (JSDS II) unaotarajiwa kuwa chanzo rasmi taarifa zote
za mashauri kuanzia Januari 01, 2020.
(Picha na Mary Gwera, Mahakama-Arusha)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni