Jumatano, 15 Januari 2020

MAHAKAMA YA HAKIMU MKAZI KISUTU YAENDELEA KUSIKILIZA MASHAURI KWA MTANDAO

Baadhi ya Wanasheria(waliokuwa mstari wa mbele) wakiwa katika chumba cha Mahakama Mtandao maarufu kama Video  Conference wakifuatilia mashauri katika chumba cha Mahakama Mtandao, kilichopo kwenye Kituo cha Habari na Mafunzo, Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam kwa kushirikiana na Gereza la Keko Jijini Dar es salaam.

Jumla ya mashauri matano yanayohusu Uhujumu Uchumi  yametajwa  leo, na kuahiirishwa hadi Januari 29, mwaka huu. 


Baadhi ya watuhumiwa waliopo nje kwa dhamana wanaokabiliwa na shitaka la Uhujumu Uchumi (walio mstari wa nyuma) katika chumba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu  cha Mahakama Mtandao, kilichopo katika Kituo cha Habari na Mafunzo , kwenye  mahakama hiyo, Jijini Dar es salaam wakifuatilia mashitaka yao. Walio mstari wa mbele ni wanasheria.

 Baadhi ya wananchi waliofika katika  Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar es salaam kutuatilia mashauri ya ndugu zao katika chumba cha Mahakama Mtandao.


Runinga kubwa iliyopo chumba cha Mahakama Mtandao katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu inayotumika kuendeshea mashauri  ikionyesha picha ya pamoja ya chumba maalumu cha kuendeshea mashauri katika Gereza la keko.

(Picha na Innocent Kansha- Mahakama).

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni