(Na Amina Ahmad - Mahakama Kuu Tanga)
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu kanda ya Tanga Mhe. Amir R. Mruma, akisaini amefanya ziara ya kikazi kanda hiyo, wiki iliyopita ambapo amefanya ukaguzi Mahakama za Mwanzo Ngomeni na Mtindiro zilizopo Wilayani Muheza, Mahakama za Mwanzo Duga na Maramba zilizopo Wilayani Mkinga, Viwanja na Majengo ya Mahakama, Ofisi za Wakuu wa wilaya ya Muheza na Mkinga.
Pia alitembelea
Mahakama
za Mwanzo Ngomeni na Mtindiro zilizopo Wilayani Muheza, Mahakama za Mwanzo Duga
na Maramba zilizopo Wilayani Mkinga, Viwanja na Majengo ya Mahakama, Ofisi za
Wakuu wa wilaya ya Muheza na Mkinga.
Jaji Mfawidhi wa
Mahakama Kuu Kanda ya Tanga, Mhe. Amir R. Mruma akisaini kitabu cha wageni
alipotembelea Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kilindi. Pembeni yake (kulia) ni Mkuu
wa Wilaya ya Kilindi, Mhe. Sauda Salim Mtondoo.
Afisa
Ardhi wa Wilaya ya Mkinga, Bwana Obedi Katonge(kushoto) akimuonesha Jaji Mfawidhi Mhe.
Amir R. Mruma (Aliyeshika nyaraka), mipaka ya kiwanja cha Mahakama ya Wilaya ya
Mkinga. Kulia ni Kaimu Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Muheza,
Mhe. Yusuph Zahoro, akifuatiwa na Afisa Tawala wa Mahakama ya Wilaya ya Muheza,
Bw. Muharami Pazzi.
Jengo
lililopatikana kwa ajili ya kuanza kutoa huduma za Mahakama ya Wilaya ya
Mkinga.
|
Jengo
lililopatikana kwa ajili ya kuanza kutoa huduma za Mahakama ya Wilaya ya
Mkinga.
(Picha na Amina Ahmad - Mahakama Kuu Tanga)
|
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni