Na Magreth Kinabo - Mahakama
Jumla ya Sheria 38 zimefanyiwa uchambuzi, sheria 20 zimepitiwa na Kamati ya Kanuni
ya Jaji Mkuu, ambapo sheria 9 zimekamilika kwa ajili ya kuisaidia Mahakama ya Tanzania kuondoka na mbinu za
kiufundi, ili kuiwezesha kutoa haki na
kumaliza mashauri kwa wakati.
Aidha kanuni 41 zimepitiwa na
kufanyiwa kazi ziko katika hatua za mwisho na kanuni 33 kutangazwa kwenye
Gazeti la Serikali kwa minajili ya kutumika.
Akizungumza na wataalamu kutoka Benki ya Dunia, (WB) leo Mjumbe kutoka Sekretarieti ya kamati hiyo, Mhe. Kifungu Mrisho, kutoka
Kitengo cha Menejimenti ya Mshauri cha Mahakama ya Tanzania alisema tayari utaratibu wa kuweka mabadiliko ya
Sheria 450 kupitia Mwanasheria Mkuu wa Serikali unaendelea.
‘‘Tumefanya maboresho ya sheria na kanuni ni kwa lengo la kurahisiha
utaratibu mzima wa uendeshaji wa mashauri kuanzia hatua ya awali ya upokelewaji
wa shauri hadi hatua ya mwisho kabisa ya utekelezaji wa tozo uliotokana na
hukumu au uamuzi ama amri ya Mahakama, alisema
Mhe. Mrisho.
Kwa upande wake Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, kutoka Masjala Kuu ambaye ni Mjumbe wa kamati
hiyo, Mhe. Faiz Twaib
alisema ‘‘Tumefanya marekebisho makubwa ya
sheria na kanuni mbalimbali, ambazo zimesaidia mashauri yaliyoko
mahakamani kumalizika kwa wakati na tumepunguza mlundikano. Hivyo kamati hii
ni moja ya kamati za Jaji Mkuu, ambayo iko hai na inatekeleza majukumu
yake mara kwa mara,’’ alisema Mhe. Twaib.
Naye Mtaalamu kutoka WB, Bw. Waleed Malik aliipongeza Mahakama kwa hatua ya
mabadiliko hayo.
Mhe. alizitaja baadhi ya sheria
zilizofanyiwa mabadiliko kuwa ni, Sheria ya Vyombo vya Habari
iliyotungwa mwaka 2017(Media Service Act of 2017),
Sheria ya Migogoro ya Ardhi Sura Namba 216 kama ilivyofanyiwa marejeo mwaka
2002 (Land Dispute Act Cap. 216 RE 2002) nayo imefanyiwa marekebisho na kuruhusu
Wahe. Mahakimu wenye mamlaka ya nyongeza kusikiliza mashauri ya migogoro ya
ardhi katika Mahakama Kuu ya Tanzania.
Nyingine Sheria za Madai na taratibu zake ya mwaka 2019, imepunguza
hatua za usikilizwaji wa mashauri ya madai kutoka hatua 38 hadi hatua 22 tu
zitakazo tumika mahakamani.
Mwaka 2016 kamati hiyo
iliweza kupendekeza mabadiliko ya Sheria Sura Namba 141 ambayo ni Sheria ya Rufani
inayotoa mamlaka ya kusajili rufaa katika Mahakama ya Rufani ambayo haikuwa na kipengele cha mapitio.
Hakimu huyo aliongeza
kwamba kamati hiyo,imefanya kazi zingine za kawaida za kuandaa maelekezo,
miongozo na waraka mbalimbali.
|
Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania
Masjala Kuu, Mhe.Faiz Twaib akizungumza
jambo. akiwa katika kikao cha tathimini utendaji kazi zilizofanywa na Kamati ya Kanuni ya Jaji Mkuu, ukiwemo ujumbe wa Benki ya
Dunia (WB). Kikao hicho kimefanyka leo kwenye ukumbi wa Maktaba ya Mahakama ya Rufani Tanzania , ambapo ujumbe WB umeipongeza kamati hiyo kwa ufanisi wa maboresho ya
sheria na kanuni ambazo zimesaidia Mahakama kuondokana na mbinu za kiufundi katika kutoa
haki kwa wananchi, ikiwemo kurahisisha umalizaji wa mashauri kwa wakati .
|
|
Wajumbe wakiwa katika kikao cha tathimini utendaji kazi zilizofanywa na Kamati ya Kanuni ya Jaji Mkuu, ukiwemo ujumbe wa Benki ya Dunia (WB). Kikao hicho kimefanyka leo kwenye ukumbi wa Maktaba ya Mahakama ya Rufani Tanzania , ambapo ujumbe wa WB umeipongeza kamati hiyo kwa ufanisi wa maboresho ya sheria na kanuni ambazo zimesaidia Mahakama kuondokana na mbinu za kiufundi katika kutoa haki kwa wananchi, ikiwemo kurahisisha umalizaji wa mashauri kwa wakati . |
Ujumbe wa Benki ya Dunia ukifuatilia tathimini hiyo.
|
Mtaalamu kutoka Benki ya Dunia, Bw. Waleed Malik (katikati) akifafanua jambo leo
katika kikao hicho, wenzake (kushot)o
ni Bi. Debohar Isser na Bi. Clara Maghani ( kulia).
|
Mjumbe wa Sekretarieti ya Kamati ya Kanuni, ambaye pia ni Hakimu Mkazi, Mhe.
Kifungu Mrisho (kushoto wa kwanza), akiwasilisha leo tathimini ya utendaji kazi zilizofanywa na Kamati ya Kanuni ya Jaji Mkuu,
katika kikao hicho kilichofanyika
kwenye ukumbi wa Maktaba ya Mahakama ya
Rufani Tanzania .
(Picha na Magreth Kinabo- Mahakama)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni