Na
Mary Gwera, Mahakama
Jaji Mkuu wa Ethiopia, Mhe.
Meaza Mengistu ameonyesha kufurahishwa na uendeshaji wa mashauri manne (4)
yaliyosikilizwa kwa njia ya video ‘Video Conference’ kati ya Mahakama ya Hakimu
Mkazi Kisutu na Gereza la Keko jijini Dar es Salaam.
Akizungumza mara baada
ya kukamilika kwa usikilizwaji wa mashauri hayo yaliyoendeshwa mapema Februari
19, 2020 na Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Mhe.
Augustina Mmbando, Jaji Mkuu huyo alisema zoezi la usikilizwaji limeenda
vizuri.
“Nimefurahishwa na
jinsi ambavyo Hakimu ameendesha kesi, ameonyesha kuwa makini na mwenye
kujiamini kwa wakati wote aliokuwa akiendesha mashauri hayo,” alisema Mhe. Jaji
Mengistu.
Mashauri yote manne yaliyosikilizwa
ni ya uhujumu uchumi, yaliyohusisha Jamhuri dhidi ya Rafael Herman na wenzake,
Jamhuri dhidi ya Raia wa China aitwaye Chen Jian Lin, Jamhuri dhidi Maarifa
Abasi Nasoro na Jamhuri dhidi ya Mohamed Yohana Mohamed.
Watuhumiwa wawili kati
ya hao wamepatiwa dhamana na wawili wamerudishwa rumande.
Aidha Wakili
Mwandamizi wa Serikali, Bw. Wankyo Simon alimweleza Hakimu huyo kuwa upelelezi
dhidi ya kesi hizo haujakamilika hivyo zimeahirishwa hadi Machi 04 mwaka huu.
Mbali na kushiriki katika uendeshaji wa mashauri hayo,
Mhe. Jaji Mengistu pamoja na Ujumbe kutoka Benki ya Dunia walipata fursa ya
kusikiliza wasilisho linalohusu Chuo cha Uongozi wa Mahakama-Lushoto lililowasilishwa
na Mkuu wa chuo hicho, Mhe. Jaji.Dkt. Paul Kihwelo.
Naye, Mkurugenzi wa
TEHAMA-Mahakama ya Tanzania, Bw. Kalege Enock aliwasilisha kwa ujumbe huo
wasilisho la Mifumo mbalimbali ya Kielektroniki inayotumika Mahakamani.
Bw. Enock aliitaja
mifumo hiyo kuwa ni pamoja na Mfumo wa Kusajili na Kuratibu Mashauri Mahakamani
(JSDS II), Mfumo wa kusajili na kuratibu Mawakili (TAMS), Mfumo wa anuani za
Kijiografia wa Mahakama (J-MAP), Mfumo wa Kiielektroniki wa kutunza maamuzi ya
Mahakama (Tanzlii) pamoja na Maktaba Mtandao (‘E-Library).
Jaji Mkuu huyo leo
amehitimisha ziara yake ya siku tatu (3) ya kuitembelea Mahakama ya Tanzania ambapo
kupitia ziara hiyo amepitishwa katika maeneo mbalimbali ya maboresho
yaliyofanywa na Mahakama nchini.
Jaji Mkuu wa Ethiopia, Mhe. Meaza Mengistu akizungumza jambo katika Kituo cha Mafunzo
na Habari za Kimahakama Kisutu ambapo jumla mashauri manne (4) yamesikilizwa.
Jaji Mkuu wa Ethiopia
pamoja na ujumbe kutoka Benki ya Dunia wakifuatilia wasilisho kutoka kwa Mkuu
wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto, Mhe. Jaji Dkt. Paul Kihwelo.
Muonekano wa picha ya
video ikionyesha mandhari ya Chuo na Wajumbe wanavyofuatilia.
Msajili, Mahakama Kuu
ya Tanzania, Mhe. Sharmillah Sarwatt (kulia) pamoja na Maafisa wengine wa
Mahakama wakifuatilia kinachojiri.
Mhe. Jaji Kihwelo
akifafanua jambo kwa Jaji Mengistu kuhusiana na Chuo cha Uongozi wa Mahakama
(IJA)-Lushoto.
Mkuu wa Kitengo cha
Maboresho- Mahakama ya Tanzania, Mhe. Zahra Maruma akizungumza jambo katika
majadiliano hayo.
Mkurugenzi wa
TEHAMA-Mahakama ya Tanzania, Bw. Kalege Enock (kushoto) akiwasilisha mada ya
maendeleo ya TEHAMA Mahakamani.
(Picha na Mary Gwera,
Mahakama)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni