Jumanne, 25 Februari 2020

JAJI KIONGOZI AZUNGUMZA NA UJUMBE WA BENKI YA DUNIA


Jaji   Kiongozi   wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt. Eliezer Feleshi ( wa kwanza kulia) akizungumza leo na ujumbe wa Benki ya Dunia (WB)  kuhusu mafanikio yaliyopatikana katika ripoti ya utafiti juu ya usikilizaji na umalizaji  wa mashauri ya jinai kwa wakati. Wa pili kulia ni Msajili  wa Mahakama Kuu  ya Tanzania, Mhe. Sharmillah Sirwatt na wengine ni baadhi ya viongozi wa Mahakama ya Tanzania.

 Aidha   Jaji Kiongozi   aliueleza ujumbe huo kuhusu mabadiliko ya sheria mbalimbali yalivyowezesha  usikilizaji  wa mashauri ya jinai kwa haraka. Ujumbe huo uko nchini kwa ziara ya kikazi.


Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania,  Mhe. Dkt. Eliezer Feleshi ( wa kwanza kulia) akifafanua jambo  leo kwa ujumbe wa Benki ya Dunia (WB)  kuhusu mafanikio yaliyopatikana katika ripoti ya utafiti juu ya usikilizaji na umalizaji  wa mashauri ya jinai kwa wakati. Wa pili kulia ni Msajili wa Mahakama  Kuu ya Tanzania, Mhe. Sharmillah Sirwatt na wengine ni baadhi ya viongozi wa Mahakama ya Tanzania.
Ujumbe wa Benki ya Dunia (WB) na baadhi ya viongozi wa Mahakama ya Tanzania wakimsikiliza Jaji Kiongozi (ambaye hayupo pichani).
Mtaalamu wa Benki ya Dunia (WB), Bi. Debohar  Isser akisisitiza jambo wakati wa mazungumzo hayo, ( wa tatu kushoto)  ni  Bi. Clara Maghani   na  (wa nne   kushoto)  ni Bw. Denis Biseko (wote ni wataalamu kutoka WB.
Mtaalamu wa Benki ya Dunia (WB), Bw. Waleed Malik (wa pili kushoto) akifafanua jambo wakati wa mazungumzo hayo.

(Picha na Magreth Kinabo – Mahakama ya Tanzania)
 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni