Jaji wa Mahakama Kuu Zanzibar Mhe. Mkusa Isaac Sepetu amefariki Dunia leo Asubuhi, Zanzibar.
Pichani ni Jaji wa Mahakama
Kuu Zanzibar Marehemu Mkusa Isaac Sepetu.
HISTORIA YA MAREHEMU MKUSA ISAAC SEPETU
(JAJI
WA MAHAKAMA KUU ZANZIBAR)
KUZALIWA
Marehemu Jaji Mkusa
Sepetu alizaliwa 12/3/1974 Zanzibar
ELIMU
Alipata Elimu yake ya Msingi
na Sekondari nchini Russia mwaka 1982-1992
Alisoma Shahada ya kwanza
ya Sheria (LLB) mwaka 1993-1997 nchini Russia
AJIRA
Mwaka 2001-2002 –
Marehemu aliajiriwa kama Afisa Sheria wa wizara ya Fedha na Uchumi Zanzibar.
Mwaka 2002-2004 - Aliteuliwa
kuwa Hakimu wa Mkoa katika Mahakama ya Mkoa wa Vuga.
Mwaka 2004-2006- Aliteuliwa
kuwa Hakimu wa Mkoa Dhamana katika Mahakama ya Mkoa wa Kaskazini Pemba.
Mwaka 2006-2009-
Aliendelea kuwa Hakimu wa Mkoa Dhamana wa Mahakama ya Mkoa wa Kusini Unguja
(Mwera)
Mwaka 2009-2010 Aliendelea
kuwa Hakimu Dhamana wa Mahakama ya Mkoa wa Vuga
2010-2020 Aliteuliwa kuwa
Jaji wa Mahakama Kuu Zanzibar.
NYADHIFA
NYINGINE ZA UTEUZI
2014-2020 Aliteuliwa kuwa
Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Mahakama Zanzibar
10/12/2014- 20/1/2015
Aliteuliwa kuwa Kaimu Jaji Mkuu wa Zanzibar
1/12/2016 -16/1/2017
Aliteuliwa kuwa Kaimu Jaji Mkuu wa Zanzibar
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni