Jumapili, 16 Februari 2020

JAJI MKUU WA ETHIOPIA AWASILI NCHINI KUJIFUNZA MABORESHO YA MAHAKAMA

Jaji Mkuu wa Ethiopia, Mhe.  Meaza Ashenafi Mengistu  (kulia) akipokelewa  leo na Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni  ya Biashara ,  Mhe. Patricia  Fikirini  mara baada ya kuwasili katika Kiwanja  cha  Ndege cha  Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam  kwa ajili ya kujifunza na kubadilishana uzoefu wa  Maboresho mbalimbali yaliyofanywa na Mahakama ya Tanzania. Jaji Mkuu wa Ethiopia amewasili nchini kwa ziara ya siku tatu. Nchi hiyo ipo katika Mpango wa Maboresho wa Huduma za Mahakama wa miaka mitatu.
Jaji Mkuu wa Ethiopia, Mhe. Meaza Ashenafi Mengistu (kulia) akisalimiana   leo na Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania , Mhe. Sharmillah Sarwatt.  mara baada ya kuwasili katika Kiwanja cha Ndege  cha   Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Jaji Mkuu wa Ethiopia, Mhe. Meaza Ashenafi Mengistu  (kulia) akisalimiana leo na  Balozi wa Ethiopia nchini Tanzania,  Mhe. Yonas Sanbe  mara baada ya kuwasili katika Kiwanja cha Ndege  cha  Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

Jaji Mkuu wa Ethiopia, Mhe Meaza Ashenafi Mengistu  (kulia) akizungumza jambo leo na  Balozi wa Ethiopia nchini Tanzania,  Mhe. Yonas Sanbe  mara baada ya kuwasili katika Kiwanja  cha Ndege cha  Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Jaji Mkuu wa Ethiopia,  Mhe.Meaza Ashenafi Mengistu   (kulia) akizungumza jambo  leo na Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni  ya Biashara , Mhe. Patricia  Fikirini  mara baada ya kuwasili katika Kiwanja  cha Ndege cha  Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

(Picha na  Magreth Kinabo-Mahakama)



Hakuna maoni:

Chapisha Maoni