Alhamisi, 6 Februari 2020

RAIS MAGUFULI AFURAHISHWA NA MABORESHO YA MAHAKAMA


Na Mary Gwera  na Magreth Kinabo, Mahakama

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ameipongeza Mahakama ya Tanzania kwa utendaji mzuri wa kazi ikiwemo matumizi  bora ya fedha za Serikali.

Akizungumza katika sherehe za kilele cha Siku ya Sheria nchini, Februari 06, 2020 katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Mwl. Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam, Mhe. Rais alionyeshwa kufurahishwa na utendaji wa Mahakama katika Maboresho yaliyofanyika ikiwemo kupunguza mlundikano na ucheleweshaji wa mashauri, matumizi ya Tehama, Huduma ya Mahakama inayotembea ‘mobile court services’, maboresho ya miundombinu ya majengo na kadhalika.

“Leo nina furaha kubwa sana, kwa kuwa Mahakama imepata mafanikio makubwa katika kipindi cha miaka minne (4) iliyopita, hivyo nakupongeza Mhe. Jaji Mkuu na Watumishi wote wa Mahakama kwa kazi nzuri ya utoaji haki nchini,” alisema Mhe. Rais.

Mbali na pongezi hizo, Mhe. Rais aliisifu pia Mahakama kwa matumizi mazuri ya fedha zinazotolewa na Serikali kwa ajili ya matumizi mbalimbali ikiwemo ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya Mhimili huo.

“Hakuna ufisadi Mahakama, fedha zinazotolewa zinatumika vizuri, hivyo nawapongeza sana,” alieleza Mhe. Dkt. Magufuli.

Aidha; Mhe. Rais aliongeza kuwa suala la ucheleweshwaji wa usikilizwaji wa Mashauri limepungua kwa asilimia 100, huku akitoa mfano kuwa katika mwaka 2016 mlundikano wa mashauri umepungua kutoka asilimia 12 hadi asilimia 5 kwa sasa.

Katika hatua nyingine, Rais Magufuli alizungumzia juu ya mafanikio ya uanzishwaji wa Mahakama Kuu-Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi maarufu kama ‘Mahakama ya Mafisadi’ kuwa Mahakama hiyo imepata mafanikio makubwa.

“Tangu Mahakama ya Mafisadi ianzishwe mwaka 2016 jumla ya mashauri ya uhujumu uchumi 119 yamesajiliwa na mashauri 89 yamemalizika ambapo faini ya sh. bil. 13.6 na fidia ya bil.30.6 zimetolewa,” alieleza.

Aliongeza kuwa uanzishwaji wa Mahakama ya Mafisadi umeondoa dhana iliyokuwa imejengeka miongoni mwa wananchi kuwa mapambano dhidi ya rushwa nchini yamekuwa yakiwalenga wananchi wa chini na kuwaacha vigogo.

Hali kadhalika Mhe. Rais amemuhakikishia Mhe. Jaji Mkuu kushughulikia changamoto zilizopo ndani ya Mahakama ikiwemo upungufu wa rasilimali watu, maslahi duni ya watumishi, pamoja na kuongeza fedha matumizi ‘OC’.

Awali akizungumza kabla ya kumkaribisha Mhe. Rais, Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma alisema Mfumo wa Kielekitroniki wa Kusajili na Kuratibu Mashauri (JSDS II) uliouzindua mwaka jana umeendelea kuwa msaada mkubwa katika kurahisisha shughuli za uendeshaji wa mashauri.

Mhe. Prof. Juma alisema kuwa mfumo huu ambao unatoa taarifa kwa wadau kwa njia ya ujumbe mfupi wa maandishi na barua pepe, umeunganishwa pia na wa malipo ya serikali (Government Electronic Payment Gateway (GEPG)) na Mfumo wa Kusimamia Mawakili (TAMS).

“Kuunganishwa Mfumo wa JSDS2 na mfumo wa malipo ya Serikali umeiwezesha Mahakama kudhibiti ukusanyaji wa Tozo na Ada. Udhibiti huu umewezesha ongezeko la maduhuli toka shilingi bilioni 1.6 mwaka 2017 mpaka shilingi bilioni 2.5,” alieleza Mhe. Jaji Mkuu.

Aliongeza kuwa katika kipindi cha mwaka jana jumla ya mashauri 2,435 yalifunguliwa kwa kielektroniki. Lengo la Mahakama ni kuendelea kuboresha mfumo kwa kutumia wataalamu wa ndani.

Siku ya Sheria nchini, ilitanguliwa na Maonesho ya Wiki ya Utoaji Elimu ya Sheria ambayo kitaifa ilifanyika kuanzia Januari 31 hadi Februari 05 mwaka huu ambapo kwa mwaka huu Kaulimbiu ni “Uwekezaji na biashara; Wajibu wa Mahakama na wadau katika kukuza uwekezaji na biashara.”.
Rais wa Jamhuri  ya  Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akitoa hotuba  yake ya Siku ya Sheria nchini iliyofanyika leo kwenye ukumbi wa mikutano wa Mwalimu J. K. Nyerere uliopo jijini Dar es Salaam.


 Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akitoa hotuba yake.
Meza kuu ikiwa katika sherehe hizo.


 Baadhi ya Watumishi wa  Mahakama ya Tanzania na wageni waalikwa wakiwa katika sherehe hizo.
Baadhi ya Watumishi wa  Mahakama ya Tanzania na wageni waalikwa wakiwa katika sherehe hizo.


 Baadhi ya Watumishi wa  Mahakama ya Tanzania na wageni waalikwa  wakiwa katika sherehe hizo.


Viongozi wa kisheria wa serikali na binafsi.
                      
Wadau wa Mahakama wakiwa katika sherehe hiyo.



Rais wa Jamhuri ya  Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Majaji wa Mahakama ya Uingereza na Taasisi ya Slynn,  wakati wa kilele cha  Siku ya Sheria nchini iliyofanyika leo kwenye ukumbi wa mikutano wa Mwalimu J.K. Nyerere uliopo jijini Dar es Salaam. 

Viongozi Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama wakiwa katika sherehe hizo.

Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe.  Wilbard Chuma (wa kwanza mstari wa pili aliyevaa joho jeusi).


Mwanasheria Mkuu wa  Serikali, Profesa  Adelardius  Kilangi akitoa hotuba.


Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS). Rugemeleza Nshala akitoa hotuba.
Rais wa Jamhuri ya  Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli (katikati) akiwa katika picha ya  pamoja  na Majaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania,  wakati wa kilele cha  Siku ya Sheria nchini iliyofanyika leo kwenye ukumbi wa mikutano wa Mwalimu J.K. Nyerere uliopo jijini Dar es Salaam.



Rais wa Jamhuri ya  Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli (katikati) akiwa katika picha ya  pamoja  na Majaji wa Mahakama  Kuu ya  Tanzania,  wakati wa kilele cha   Siku  ya Sheria nchini iliyofanyika leo kwenye ukumbi wa mikutano wa Mwalimu J.K. Nyerere uliopo jijini Dar es Salaam.


Rais wa Jamhuri ya  Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli (katikati) akiwa katika picha ya  pamoja  na  baadhi ya vioongozi wa kisiasa,  wakati wa kilele cha  Siku ya Sheria nchini iliyofanyika leo kwenye ukumbi wa mikutano wa Mwalimu J.K. Nyerere uliopo jijini Dar es Salaam.

Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma ( wa kwanza kushoto) akitoka nje na Majaji kwa ajili ya kukagua gwaride maalum.

                                                   Gwaride maalum.

Bendi ya polisi.


Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akikagua  gwaride maalum.

Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akikagua  gwaride maalum.
Viongozi  wa Mahakama ya Tanzania walioteuliwa hivi karibuni na Rais. Kulia ni  Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Wilbard  Chuma akizungumza  jambo na Msajili wa Mahakama ya Rufani Tanzania, Mhe. Kevin Mhina (katikati) na kushoto ni Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Sharmillah Sarwatt.

Baadhi ya waandishi wa habari wakichukua matukio.
 Kwaya ya Mahakama ya Tanzania ikitumbuiza.

( Picha na Magreth Kinabo- Mahakama)




Hakuna maoni:

Chapisha Maoni