JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
TAARIFA
KWA UMMA
TAHADHARI YA UGONJWA WA CORONA
Dar
es Salaam: Machi 18, 2020
Watumishi
wa Mahakama na wananchi wote.
Kama mnavyofahamu ugonjwa
wa COVID-19 unaenea kwa kasi duniani. Kwa hapa nchini tayari imeshathibitishwa
kuwepo kwa ugonjwa huu. Lakini pia katika nchi jirani za Kenya na Rwanda kuna
taarifa za kuongozeka kwa wagonjwa wa “Corona Virus”. Mahakama ya Tanzania
inaungana na Serikali katika mapambano dhidi ya ugonjwa huu.
Hivyo; Uongozi wa Mahakama
unawataka Watumishi, wateja wa Mahakama na wananchi kwa ujumla kuzingatia
yafuatayo:-
(i)
Endapo
wewe sio sehemu ya kesi/shauri unaombwa kutohudhuria katika kesi hadi hapo
itakapo tangazwa vinginevyo.
(ii)
Kila
mmoja (watumishi na wadau) kabla ya kuingia kwenye ofisi au kumbi za Mahakama
anatakiwa kunawa mikono na kujipaka dawa maalum (sanitizer) ambazo zitakuwa
zimeweka katika milango au mageti ya Mahakama husika.
(iii) Epuka
kusalimiana kwa kushikana mikono, kukumbatiana au kubusiana.
(iv)
Tafadhali
zingatia tahadhari nyingine ambazo zimetolewa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya
Jamii, Wazee, Jinsia na Watoto.
Imetolewa na:
Wanyenda
Ph. Kutta
Kny: Mtendaji Mkuu,
Mahakama ya Tanzania
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni