Na Innocent Kansha –
Mahakama.
Jumla ya washiriki 49
kutoka mikoa mbalimbali nchini wameanza mafunzo ya siku tano yanayofanyika
Mjini Morogoro kuanzia Machi 16 hadi 20, mwaka huu kwa lengo la kujengewa uwezo
wa kuripoti habari zinazohusu Mahakama ya Tanzania kwa usahihi.
Mafunzo haya
yanafanyika kwa makundi mawili tofauti ambayo ni Wahariri wa Habari (Sub
Editors) pamoja na Maafisa wa Mahakama ambao ni wawakilishi wa Maafisa Habari
wa Mahakama ya Tanzania kutoka mikoa mbalimbali nchini.
Akifungua mafunzo hayo
Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, ambaye ni Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa
Mahakama Lushoto (IJA), Mhe. Dkt. Paul Kihwelo alisema Mahakama ya Tanzania inatambua
mchango mkubwa wa wanahabari kama isemavyo nguzo ya tatu ya Mpango Mkakati wa
Mahakama ya Tanzania wa Miaka Mitano (2015/2016
hadi 2019/2020).
“Mahakama inatambua
umuhimu wa habari na wanahabari na Maafisa Habari wa Mahakama wana nafasi kubwa
ya kuieleza jamii mambo yanayoendelea mahakamani, sio tu kueleza mambo ya mahakama
ila kueleza taarifa za Mahakama kwa
usahihi,”. alisema Jaji Kihwelo.
“Mafunzo haya yaliwekwa
kwa miaka miwili mfululizo ikiwa ni sehemu ya kutekeleza mpango huo, na hili ni
eneo muhimu kupita nguzo ya tatu
inayosisitiza Kujenga imani kwa wananchi na ushirikishwaji wa wadau katika mpango huu,” alisema Jaji Kihwelo.
Jaji Kihwelo
alisisitiza kwamba mafunzo hayo yana lengo la kufanya tathimini ya mafunzo yaliyotolewa awali ili kujipanga kwa mafunzo
yanayotolewa sasa na jinsi gani ya
kujipanga vizuri kwa mafunzo yatakayofanyika baade.
Mahakama mara nyingi
huzungumuza au kutoa maamuzi kupitia kalamu na Jaji au Hakimu hawezi kutoka
mbele ya umma kutetea uamuzi wake kwa umma hii ni kutokana na mfumo wa
kitaasisi, hii imekuwa na mijadala mingi sio kwa Tanzania tu hata duniani kote
ndio inatufanya tuwe na Maafisa Habari ili waweze kutoa ufafanuzi wa hali kama hizi za
sintofahamu, alifafanua Jaji Kihwelo.
Aidha, alisema kuwa
watu wengi hawajui mifumo ya mahakama inavyofanya kazi kutoka ngazi moja kwenda
nyingine. Hali inayosababisha wakati wanapokosoa kutofanya katika misingi iliyo
sahihi, hivyo mafunzo haya yatasaidia kutengeneza njia bora ya kutatua changamoto
kama hizo.
Washiriki wa mafunzo
ambao ni Maafisa wa Mahakama ya Tanzania wanaowakilisha kada ya Maafisa Habari wa Mahakama ya Tanzania kutoka
mikoa mbalimbali nchini.
|
Na Innocent Kansha –
Mahakama.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni