Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma kwa mara ya kwanza amewafanyia usaili wahitimu wa taaluma ya Sheria kwa ajili ya kuwapokea na kuwakubali kuwa Mawakili kwa njia ya Mtandao ‘Video Conference’.
Akizungumzia kuhusu usaili huo, Naibu
Msajili Mwandamizi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala Kuu, Mhe. Messe Chaba,
alisema usaili huo unafanyika baada ya wahitimu hao, kufanya maombi ya kukubaliwa kuwa
mawakili kwa mtandao na kukidhi vigezo
vinavyotakiwa na Baraza la Elimu ya Sheria.
‘‘Tumetumia njia hii ya mtandao ili
kuendena na mabadiliko ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) na kuliishi
agizo la Jaji Mkuu alilolitoa katika
hotuba yake ya kilele cha Siku ya Sheria nchini Februari Mosi, mwaka 2018, ambapo
aliwataka Majaji, Mahakimu na Watumishi wa Mahakama kubadili fikra na mtazamo
ili kujiandaa na kujiimarisha kwenye matumizi ya TEHAMA katika karne hii ya 21,
ikiwa ni hatua ya kurahisisha utendaji kazi wetu. Tumefanikiwa kutumia njia vizuri
kwa siku na tuna wahitimu takribani 80
wanaofanyiwa usaili, ’’ alisema Mhe. Chaba.
Alisema usaili huo, umeanza kufanyika Juni 23, mwaka huu na utamalizika
Julai 3, mwaka huu.
Chaba ambaye pia Katibu wa Baraza la Elimu ya Sheria, alisema njia hiyo ina
faida kwa wanataaluma hao, kwa kuwa inawapunguzia gharama za usafiri, malazi, muda
na usumbufu unaoweza kujitokeza wakati
wa wa kusafiri Jijini Dar es Salaam ili kufika kwenye ofisi za Jaji Mkuu kwa
ajili ya kufanyiwa usaili huo.
Aliongeza kuwa usaili huo umekuwa ni fursa kwa Mahakama kwa
kuwa umeongeza matumizi ya TEHAMA hususan kipindi ambacho dunia na nchi
ya Tanzania inakumbwa na janga la ugonjwa wa homa kali ya mapafu, COVID 19 unaosababishwa na virusi vya Corona, ikiwa ni hatua mojawapo za
kuepuka maambukizi dhidi ya tatizo hilo.
‘‘Mchakato wa kuwapata wanataaluma hao ulifanyika mwezi Aprili na Mei,
lakini hufanyika mara mbili kwa mwaka, ambapo
utafanyika tena Novemba na Desemba mwaka huu. ‘‘Wanataaluma hawa walituma maombi
katika baraza hili, kuanzia Aprili Mosi mwaka huu hadi Mei 14, mwaka huu kwa
ajili ya kuomba kuwa mawakili, hivyo jumla yao walikuwa 651 na waliokidhi
vigezo ni takribani 613 ambao ndio tunawafanyia usaili,’’ alisema Mhe. Chaba.
Alivitaja baadhi ya vigezo vya kukubalika katika usaili huo ni kuleta maombi,
kumaliza Shule ya Sheria (Law School), kuwasilisha vyeti, kupitia elimu
ya Diploma ya Sheria, Elimu ya Sheria ya Chuo Kikuu, kuleta matokeo ya taaluma hiyo, kuwa na tabia njema, hati ya
kiapo cha majina, na barua ya utambulisho wa kazi.
Wanataaluma hao baada ya kumaliza usaili na kufaulu,wanatarajiwa kukubaliwa na kupokelewa kuwa Mawakili kwenye Sherehe ya 62 itakayofanyika Julai 10, mwaka huu. Aidha, mawakili hao wakishakubaliwa wataingizwa katika Mfumo wa Kusimamia Mawakili (TAMS). Sherehe hizo zilianzishwa rasmi mwaka 1986.
Wanataaluma hao baada ya kumaliza usaili na kufaulu,wanatarajiwa kukubaliwa na kupokelewa kuwa Mawakili kwenye Sherehe ya 62 itakayofanyika Julai 10, mwaka huu. Aidha, mawakili hao wakishakubaliwa wataingizwa katika Mfumo wa Kusimamia Mawakili (TAMS). Sherehe hizo zilianzishwa rasmi mwaka 1986.
Maeneo yanayotumika kufanya usaili
huo ni Mahakama Kuu ya Tanzania, Dar es Salaam watahiniwa (438),
Arusha (46), Tanga (watano), Tabora (16), Mtwara (watatu), Dodoma (23), Mbeya (27)
na Mwanza (44). Awali wanataaluma wa fani ya Sheria walikuwa wakikutana na Jaji Mkuu ana kwa ana kufanyiwa usaili.
Jaji
Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akiwa ofisini kwake Jijini Dar
es Salaam akimfanyia usaili mhitimu wa
Shule ya Sheria kwa njia ya mtandao maarufu kama ”Video
Conference” ikiwa ni maandalizi ya kuapishwa kuwa Wakili .
Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim
Hamis Juma akiwa ofisini kwake Jijini Dar es Salaam akimfanyia usaili
mhitimu wa Shule ya Sheria kwa njia ya mtandao maarufu kama ”Video Conference”
ikiwa ni maandalizi ya kuapishwa kuwa Wakili .
Moja
ya Mtahiniwa aliyehitimu Shule ya Sheria akiwa kwenye chumba cha usaili Jijini Dar es Salaam kilichoko Mahakama Kuu ya Tanzana akiongozwa na Naibu Msajili Mwandamizi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala Kuu, Mhe. Messe Chaba.
Moja ya Mtahiniwa aliyehitimu Shule ya Sheria akiwa kwenye chumba cha usaili kilichoko Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Tabora. |
Baadhi
ya wahitimu wa Shule ya Sheria wakiwa wameketi kwenye chumba maalumu, Jijini
Dar es Salaam wakisubiri kufanyiwa usaili na Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof.
Ibrahim Hamis Juma.
|
Mahakama mnakwenda speed kubwa kwenye matumizi ya technology. Bila hivyo inamaana hao waliopo Tabora wangelazimika kuna dsm kuonana na Jaji Mkuu uso kwa uso!! Tunaona mageuzi makubwa mnakwenda na speed ya Chuma chetu Rais wetu JPM!! Hongereni sana Mahakama
JibuFutaAsante sana kwa pongezi.Mungu akubariki
JibuFutaHongera sana Mahakama mmekuwa kinara kwa kuonyesha mfano mzuri wa namna ya kutumia mtandao. Kumbe pana umuhimu mkubwa wa kuimarisha tekinolojia hii kote nchini ili isiwe kwa mahakama tu, itumike hata kwenye mifumo ya elimu ya chini pia. Hongera sana.
JibuFutaTunashukuru kwa pongezi
JibuFuta