Na. James Kapele –
Katavi
Jaji
Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Sumbawanga, Mhe. David Mrango
ametoa ushauri wa kuundwa kwa kamati ndogo za maadili zitakazotumika kama
jukwaa la kushauriana miongoni mwa watumishi hasa katika masuala yanayohusu
ukiukwaji wa maadili ya Utumishi wa Umma.
Mhe,
Jaji Mrango akizungumza na Watumishi wa Mahakama mkoani Katavi ametoa rai hiyo kwenye
kikao kilichofanya jana katika ukumbi wa
wazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Katavi.
Alisema
lengo la kamati hizo, ni kushauriana pindi inapotokea mtumishi kwenda kinyume
na maadili na taratibu za kiutumishi badala ya kusubiri kamati za maadili za
Mahakimu zinazosimamiwa na wakuu wa Wilaya na Mikoa.
“Kila
mtu anao wajibu wa kuwa mwaminifu katika majukumu yake ya kila siku kwa kuwa
hakuna anayependa kumuona mtumishi akipata matatizo kazini, nawashauri muone
uwezekano wa kuanzisha kamati ndogo ndogo za maadili zitakazowasaidia
kushauriana miongoni mwenu hasa pale mnapoona mwenzenu anakwenda kinyume cha
maadili na kanuni,” alisema Jaji Mrango.
Aidha
amewasisitiza watumishi hao, kuhakikisha wanaitumia Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
(TEHAMA) ipasavyo na kila mtumishi ahakikishe anakwenda sambamba na mabadiliko
hayo.
Jaji
huyo aliwataka Mahakimu kujituma na
kuhakikisha wanamaliza mashauri waliyopangiwa kuyasikiliza kwa kuwa kila Hakimu
anapimwa kwa ubora wa maamuzi anayoyatoa na idadi ya uwingi wa mashauri anayayomaliza.
Akisisitizia
ubora wa maamuzi hayo, kwa Mahakimu amewakumbusha kujiandaa kikamilifu kusikiliza mashauri
ya uchaguzi utakofanyika mwaka huu.
Alisema
mashauri hayo yanahitaji kila mmoja wetu kuwa na utayari kupitia sheria mbalimbali za uchaguzi.
Naye
Mtendaji wa Mahakama ya Mkoa wa Katavi, Bw. Epaphras Tenganamba amemshukuru,
Jaji Mrango kwa ushauri huo na kuahidi kuyafanyia kazi maagizo hayo.
Mhe. Jaji Mrango alifanya kikao hicho, baada ya kuhitimisha usikilizwaji wa mashauri ya mauaji mahakamani hapo,yaliyoanza Juni 22 hadi Julai 13, mwaka huu na kusikiliza mashauri tisa.
Mtendaji
wa Mahakama Bw. Epaphras Tenganamba aliyesimama kulia akitoa
ufafanuzi kwenye kikao hicho.
|
Baadhi ya Watumishi wa Mahakama Mkoani Katavi waliohudhuria kikao hicho. |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni