Mahakama
ya Tanzania inaendeleza kwa kasi ujenzi wa majengo ya vituo sita Jumuishi vya
utoaji haki katika mikoa mitano nchini ikiwa ni hatua ya Mhimili huo ya
kusogeza huduma karibu zaidi na wananchi.
Ujenzi
wa majengo hayo umeanza mwezi Januari mwaka huu na unatarajiwa kukamilika ifikapo
mwezi Octoba mwaka huu.
Majengo
ya Vituo Jumuishi vya utoaji haki yatakuwa na na sakafu nne yaani gorofa 3 na yatajumuisha
ngazi zote za Mahakama kuanzia Mahakama Kuu mpaka Mahakama ya Mwanzo pamoja na ofisi
za baadhi ya wadau wa Mahakama wakiwemo Polisi, Ustawi wa Jamii, Mawakili na
Waendesha Mashitaka.
Majengo
hayo yameanza kujengwa katika miji ya Arusha, Mwanza, Dodoma, Morogoro na Dar
es Salaam katika wilaya za Kinondoni pamoja na Temeke.
Kusudi la kuweka ngazi zote za Mahakama ndani ya jengo moja pamoja na ofisi za wadau ni kurahisisha mchakato wa upatikanaji wa haki pamoja na kumpunguzia mwananchi gharama.
Mahakama ya Tanzania inashirikiana na Benki ya Dunia katika ujenzi huo. Lengo la Mahakama ni kuwa na huduma ya Mahakama Kuu katika kila mkoa, Mahakama za Hakimu Mkazi katika kila Mkoa, Mahakama za Wilaya kwenye kila Wilaya na Mahakama za Mwanzo kwenye kila Tarafa kulingana na upatikanaji wa rasilimali fedha.
Ujenzi wa jengo la kituo Jumuishi cha Utoaji haki katika Mkoa wa Arusha ukiendelea.
Ujenzi wa jengo la kituo Jumuishi cha Utoaji haki katika Mkoa wa Dodoma ukiendelea.
Ujenzi wa jengo la kituo Jumuishi cha Utoaji haki katika Mkoa wa Dar es salaam wilaya ya Kinondoni ukiendelea.
Ujenzi wa jengo la kituo Jumuishi cha Utoaji haki katika Mkoa wa Dar es Salaam wilaya ya Temeke ukiendelea.
Ujenzi wa jengo la kituo Jumuishi cha Utoaji haki katika Mkoa wa Morogoro ukiendelea.
Ujenzi wa jengo la kituo Jumuishi cha Utoaji haki katika Mkoa wa Mwanza ukiendelea.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni