Na Lydia Churi-Mahakama
Jaji Mkuu wa Tanzania
Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma amemtaka Hakimu Mkazi Mfawidhi mpya wa Mahakama
ya Hakimu Mkazi Shinyanga Mhe. Mary Peter Mrio kushirikiana na viongozi wa mkoa
huo anapotekeleza majukumu yake ya utoaji haki.
Akizungumza wakati wa
hafla ya kumkabidhi hati ya uteuzi (Instrument) Hakimu huyo ambaye alimteua hivi
karibuni kuwa Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Shinyanga, Jaji Mkuu amesema
mihimili yote ya dola haina budi kushirikiana bila ya kuingiliana mipaka yake.
“Zingatia Mpango Mkakati
wa miaka mitano wa Mahakama ya Tanzania unapotekeleza majukumu yako ya kila
siku na pia uisome na kuifahamu vizuri Dira ya Taifa ya Maendeleo ya 2025”,
alisisitiza Jaji Mkuu.
Alisema Mahakama ya
Tanzania imefanya na inaendelea kufanya maboresho mbalimbali ya huduma zake
hivyo Hakimu huyo hana budi kuhakikisha maboresho hayo yanaelezwa kwa wnanchi walio
wengi ili waweze kufahamu huduma mbalimbali zinazotolewa na Mahakama.
“Mambo mengi mazuri
tumeyafanya hivyo tunapaswa kuyaeleza, mitandao
ya kijamii itumike zaidi kuwaelimisha wananchi juu ya mipango mizuri ya
Mahakama”, alisema.
Aidha, Jaji Mkuu alimtaka
Mhe. Mrio kujiepusha na migongano inayoweza kutokea katika kutekeleza shughuli za
utoaji haki na zile za Mahakama za kiutawala.
Kabla ya kuteuliwa kuwa Hakimu
Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Shinyanga, Mhe. Mrio alikuwa ni Hakimu
Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu.
Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma (katikati) akizungumza wakati wa hafla ya kumkabidhi hati ya Uteuzi (Instrument)) Hakimu Mkazi Mfawidhi Mpya wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Shinyanga Mhe. Mary Peter Mrio leo jijini Dar es salaam. Wa pili kushoto ni Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Bw. Mathias Kabunduguru.
Hakimu Mkazi Mfawidhi Mpya wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Shinyanga Mhe. Mary Peter Mrio akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Viongozi wa Mahakama ya Tanzania leo baada ya kukabidhiwa hati ya uteuzi (Instrument).
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni