Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo Kinondoni Mhe. Rukia Juma Katembo enzi ya Uhai wake.
Hakimu
wa Mahakama ya Mwanzo Kinondoni Mhe. Rukia Juma Katembo amefariki Dunia leo
Septemba 15, 2020 katika hospitali ya Ocean Road jijini Dar es salaam alikokuwa
akipatiwa matibabu.
Mwili
wa Marehemu utazikwa leo saa 10:00 jioni katika makaburi ya Kisutu jijini Dar
es salaam. Dua ya kumuombea imefanyika saa 4:00 Asubuhi, nyumbani kwake Pugu
Dampo Dar es salaam.
Marehemu
Rukia Juma Katembo alizaliwa Desemba 1 mwaka 1962. Aliajiriwa na Mahakama ya
Tanzania Julai 1 mwaka 1983. Vituo vya kazi alivyowahi kufanyia kazi ni pamoja
na Kigamboni, Temeke, Buguruni, Ilala, Pangani, Magomeni, na Kinondoni ambapo
ndiyo kituo chake cha mwisho cha kazi.
Marehemu
alikuwa akisumbuliwa na matatizo ya Nyonga na alikuwa akitibiwa katika hospitali
mbalimbali jijini Dar es salaam zikiwemo Muhimbili na Ocean Road hadi alipofariki Dunia leo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni