Alhamisi, 1 Oktoba 2020

UJENZI WA VITUO JUMUISHI VYA UTOAJI HAKI KINONDONI NA TEMEKE WAENDELEA

Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Bw. Mathias Kabunduguru (aliyenyoosha mkono juu) akielezea jambo mbele ya timu ya mainjinia wakati walipofanya ukaguzi  katika moja ya Vituo Jumuishi cha Utoaji haki (IJC) kinachoendelea kujengwa katika Manispaa ya Kinondoni Jijini Dar es salaam. Bw. Kabunduguru alifanya ukaguzi wa jengo hilo Oktoba mosi lengo likiwa ni kujionea maendeleo ya ujenzi. 

Pichani ni muonekano wa jengo la Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki (IJC) lilichopo katika ujenzi, jengo linajengwa katika Manispaa ya Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Bw. Mathias Kabunduguru akiwa ameambatana na Mkuu wa kitengo cha usimamizi wa Majengo ya Mahakama ya Tanzania Eng. Khamadu Kitunzi (kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa Habconsult Ltd Bw. Habib Nuru (kushoto) wakati wa zoezi la kukaguzi wa jengo la kituo jumuishi cha utoaji haki kinachoendelea kujengwa Manispaa ya Temeke. Mtendaji Mkuu alipata fursa pia ya kukagua jengo la Kituo Jumuishi cha Temeke.

Mhandisi kutoka 'Hainan International Ltd' , Eng. Greyson Kampuni inayojenga Vituo Jumuishi vya Utoaji Haki vya Kinondoni na Temeke akiwaonyesha Wajumbe wa Menejimenti ya Mahakama Kuu ya Tanzania jengo hilo lililopo katika ujenzi, kwa mujibu wa Mhandisi huyo ujenzi wa kituo hicho unatarajiwa kukamilika Desemba mwaka huu, 2020.

Sehemu ya Maafisa kutoka Mahakama Kuu ya Tanzania, Naibu Wasajili na Watendaji wakipata maelezo kutoka kwa Mhandisi Greyson pindi walipotembelea kukagua maendeleo ya ujenzi wa Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki Kinondoni.

Wajumbe wa Menejimenti ya  Mahakama Kuu ya Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kukagua jengo la 'IJC' linalojengwa katika Manispaa ya Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Mkuu wa kitengo cha usimamizi wa Majengo ya Mahakama ya Tanzania Eng. Khamadu Kitunzi (aliyenyoosha mkono) akiwaeleza jambo Wajumbe wa Menejimenti kutoka Mahakama Kuu ya Tanzania-Dar es Salaam pindi walipotembelea jengo la Kituo cha Haki Jumuishi kilichopo katika Manispaa ya Wilaya ya Temeke.
Lengo la ziara hizi walizofanya Mtendaji Mkuu na Menejimenti ya Mahakama Kuu-Dar es Salaam ni kuangalia maendeleo ya ujenzi wa vituo hivyo vyenye lengo la kusogeza huduma ya haki karibu zaidi na wananchi.



Hakuna maoni:

Chapisha Maoni