TANZIA
MWILI WA MAREHEMU UTASAFIRISHWA USIKU
WA KUAMKIA TAREHE 8/10/2020 KUREJESHWA NYUMBANI KWAO ENEO LA IWAMBI/TAZARA
MAZIWA, JIJINI MBEYA KWA AJILI YA KUAGWA KABLA YA KUSAFIRISHWA KWENDA UWANJI WILAYANI
MAKETE MKOANI NJOMBE KWA MAZISHI.
MAREHEMU ALIAJIRIWA KAMA HAKIMU WA
MAHAKAMA YA MWANZO NA KUFANYA KAZI KATIKA KITUO CHA MAHAKAMA YA MWANZO CHUNYA
MJINI KUANZIA DESEMBA, 2007 MPAKA MAUTI YALIPOMKUTA USIKU WA KUAMKIA LEO.
AIDHA, KABLA YA KUWA HAKIMU WA MAHAKAMA YA MWANZO, MAREHEMU ALIWAHI KUFANYA KAZI MAHAKAMA YA TANZANIA KATIKA KITUO CHA MAHAKAMA KUU MASJALA YA MBEYA KAMA KARANI MSAIDIZI DARAJA LA I, CHEO ALICHOKITUMIKIA MPAKA DESEMBA 2007 ALIPOBADILI KADA NA KUWA HAKIMU WA MAHAKAMA YA MWANZO. MAREHEMU AMEACHA MKE NA WATOTO WATATU.
BWANA ALITOA, BWANA AMETWAA, JINA LAKE LIHIMIDIWE.
Mhe. Zakoleo Lameck Sanga enzi ya Uhai wake.
Pumzika kwa amani msomi. Njia yako njia yetu.
JibuFuta