Na Amina Ahmad, Mahakama Kuu-Tanga
Wakazi
wa Jiji la Tanga na wananchi wote kwa ujumla wameshauriwa kujenga utamaduni wa
kujifunza masuala ya kisheria ili kuweza kufahamu na kutambua haki zao.
Jaji
wa Mahakama Kuu Kanda ya Tanga, Mhe. Edson Mkasimongwa aliyasema hayo hivi
karibuni alipokuwa akitoa elimu ya sheria kwa wananchi/wateja wa Mahakama waliofika
kupata huduma mbalimbali za kimahakama katika Mahakama hiyo.
“Katika
kipindi hiki ambacho watoto wetu watakuwa wamemaliza darasa la saba, wakati
wakisubiria matokeo yao, ni vema wazazi mkapanga hata siku moja kuja nao hapa
Mahakamani angalau na wao wakapata mawili matatu yanayohusu masuala ya sheria,” alisema Jaji Mkasimongwa.
Kwa
upande wao baadhi ya wananchi waliobahatika kupata elimu iliyotolewa na Mhe. Jaji waliipongeza
Mahakama kwa kuanzisha mpango wa kuwaelimisha kuhusu masuala ya kisheria
kuiomba Mahakama kuangalia namna ya kufanya lugha ya Kiswahili itumike kuandaa
Mienendo ya kesi pamoja na Hukumu kuanzia ngazi ya Mahakama za Wilaya mpaka
ngazi ya Mahakama ya Rufani.
Wananchi
hao walitoa maoni yao juu ya kusambaza vipeperushi vya Mahakama vya kutosha ili
kuwafikia watu wengi hasa wale waliopo vijijini.
Huu
ni mwendelezo wa utoaji Elimu ya sheria kwa Umma, ambapo wananchi hao walipata
elimu juu ya utaratibu wa ufunguaji wa Mashauri Mahakamani. Aidha, katika zoezi
hilo, Mhe. Jaji Mkasimongwa aliambatana na Bi. Nakijwa Kachua, Msaidizi wa
kumbukumbu wa Kanda hiyo.
Mahakama nchini imejiwekea utaratibu wa kutoa elimu ya sheria kwa wateja wake ili kuwawezesha wananchi kuwa na uelewa wa masuala na taratibu mbalimbali za kisheria zitakazowawezesha kujua nini cha kufanya pindi wanapotafuta huduma ya haki.
Pichani ni Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Tanga, Mhe. Edson Mkasimongwa akitoa Elimu ya sheria kwa wananchi waliofika Mahakamani kwa ajili ya kupata huduma mbalimbali.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni