Jumanne, 15 Desemba 2020

MAENDELEO YA UJENZI WA VITUO JUMUISHI VYA UTOAJI HAKI ‘IJC’s’

 Muonekano katika picha, maendeleo ya ujenzi wa Vituo Jumuishi vya Utoaji Haki ‘IJC’s’ katika mikoa ya Dodoma, Arusha, Morogoro, Mwanza, Kinondoni na Temeke.

Kwa mujibu wa Bw. Fabian Kwagilwa, Mhandisi Ujenzi-Mahakama ya Tanzania amesema kwa sasa hatua ya ujenzi iliyofikiwa katika vituo hivyo ni ya umaliziaji 'finishing' na kazi za nje 'external works' na ujenzi wa vituo hivyo unatarajiwa kukamilika hivi karibuni.

Ujenzi wa Vituo hivi utakapokamilika, utasaidia kurahisisha na kusogeza huduma ya haki karibu zaidi na wananchi, aidha katika vituo hivi kutakuwa na huduma mbalimbali za haki zote zikiwa zinatolewa ndani ya jengo moja. Ndani ya majengo hayo kutakuwa na ofisi za Magereza, Mawakili na wadau wengineo.

                           Hatua iliyofikiwa ujenzi wa 'IJC' Morogoro.

 

Muonekano wa jengo la Kituo Jumuishi cha utoaji haki 'Integrated Justice Centre' -Arusha.

Muonekano wa 'IJC' Dodoma.

Hatua iliyofikiwa ujenzi wa 'IJC' Kinondoni-Dar es Salaam.

Kazi ya ujenzi ikiendelea 'IJC' Mwanza.

 'IJC' Temeke-Dar es Salaam.

 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni