Na Innocent Kansha
Jaji Mkuu wa Tanzania,
Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma amewakabidhi Mahakimu Wakazi Wafawidhi wawili wa
mikoa ya Geita na Iringa Hati au nyenzo za kuwawezesha kutekeleza majukumu yao ya
Uhakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama za Hakimu Mkazi.
Akizungumza katika hafla ya
kukabidhi Hati iliyofanyika Ofisini kwake Jijini Dar es salaam leo Desemba 22,
2020 Jaji Mkuu amewataka Mahakimu hao kwenda kusimamia utendaji wa kazi za Mahakama
za kila siku na nidhamu za watumishi katika maeneo yao ya kiutawala.
“Mmeaminiwa na utawala, nataka
mkawe mfano kwenye suala la usimamizi wa maboresho na uwekezaji mkubwa wa
mifumo yetu ya Teknologia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) katika mikoa yenu”,
alisema Mhe. Jaji Prof. Juma.
Mahakama imefanya
uwekezaji mkubwa na maboresho mbalimbali katika nyanja ya TEHAMA, imeweka
mifumo mingi ya kusaidia kurahisisha utoaji haki, kama vile Mfumo wa uhuishaji
na kusajili mashauri Mahakamani JSDS II, Mahakama Mtandao maarufu kama “Video
Conference”, Kusajili mashauri kwa njia ya mtandao “E – Failing” na mfumo wa
kutambua Mahakama “Judicial Maping”.
Aidha, Mhe. Jaji Mkuu
aliwasisitiza kusimamia kwa karibu matumizi ya mifumo hiyo ili iweze kuleta matokeo
chanja katika utendaji kazi.
Mhe. Jaji Mkuu alisema bado kuna changamoto mbalimbali katika suala la uchakataji wa takwimu sahihi za mashauri kupitia mfumo wa JSDS II, pia bado wadau wanasajili mashauri kwa njia ya kawaida mahakamani, tilieni mkazo kwenye maeneo hayo ili maboresho haya yalete maana katika utendaji wa kazi.
Mahakimu Wakazi Wafawidhi
wapya wakiwa kwenye hafla ya kukabidhiwa hati kulia ni Mhe. Said Ally Mkasiwa ambaye
amekabidhiwa hati ya kwenda kuwa Hakimu Mfawidhi Mahakama ya Hakimu Mkazi
Iringa, kushoto ni Mhe. Cleofas Frank Waane ambaye pia amekabidhiwa hati ya
kwenda kuwa Hakimu Mfawidhi Mahakama ya Hakimu Mkazi Geita wakiwa katika picha
ya pamoja
Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe.
Prof. Ibrahim Khamis Juma akisaini hati ya kuwakabidhi Mahakimu Wakazi Wafawidhi
wapya. Hafla hiyo limefanyika leo Desemba
22, 2020 katika Ofisi yake Jijini Dar es Salaam.
Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe.
Prof. Ibrahim Khamis Juma akimkabidhi Hati Mhe. Said Ally
Mkasiwa kwenda kuwa Hakimu Mfawidhi Mahakama ya Hakimu Mkazi Iringa.
Jaji
Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Khamis Juma, (wa pili kushoto) akiwa na Jaji
Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Dkt. Eliezer Mbuki Feleshi wakiwa
katika picha ya pamoja na Mahakimu Wakazi
Wafawidhi katika hafla ya kuwakabidhi Hati.
Jaji
Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Khamis Juma (watatu kushoto), Jaji Kiongozi
wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Dkt. Eliezer Mbuki Feleshi (wa tatu kulia),
Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Mhe. Wilbert Chuma (wa kwanza kushoto),
Msajili wa Mahakama ya Rufani Mhe. Kevin Mhina (wa pili kulia), Msajili wa
Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Sharmillah Sarwatt (wa kwanza kulia) wakiwa
katika picha ya pamoja na Mahakimu Wakazi Wafawidhi mara baada ya kukabidhiwa
hati.
Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Mhe. Wilbert Chuma (aliyesimama) akitoa muongozo wa namna ya kukabidhi Hati kwa Mahakimu Wakazi Wafawidhi wapya wakati wa hafla, kulia ni Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt. Eliezer Mbuki Feleshi, wa pili kushoto ni Msajili wa Mahakama ya Rufani, Mhe. Kevin Mhina na wa kwanza kulia ni Mtendaji wa Mahakama Kuu Bw. Leonard Magacha
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni