Na Mwandishi Wetu- Mahakama
Kamati ya nidhamu ya Maafisa wa Mahakama imekutana na
kuwaachia huru Maafisa watatu wa
Mahakama waliofikishwa mbele ya kamati hiyo wakituhumiwa kwa makosa mbalimbali
ya ukiukwaji wa maadili kazini.
Kwa mujibu wa Katibu wa kamati hiyo ambaye pia ni
Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Sharmilla Sarwatt, kamati hiyo
ilikutana jijini Dar es salaam kuanzia Desemba 12 hadi 14, 2020 ili kusikiliza
mashauri 13 yaliyowasilishwa.
Aidha, kati ya mashauri 13 yalisikilizwa kwenye kikao
cha kamati hiyo chini ya Mwenyekiti wake Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya
Tanzania Mhe. Dkt. Eliezer Feleshi, ni mashauri matatu 3 tu ndiyo yaliyomalizika
na kutolewa uamuzi ambapo washitakiwa wote watatu hawakutiwa hatiani
Mashauri mengine 10 bado yanaendelea kusikilizwa na
kamati hiyo.
Kwa mujibu wa Sheria ya Uendeshaji wa Mahakama namba 4
ya mwaka 2011, Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania ndiye Mwenyekiti wa
kamati hiyo na Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania ni Katibu wa kamati hiyo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni