Ijumaa, 29 Januari 2021

MAHAKAMA YAENDELEA KUTOA ELIMU WIKI YA SHERIA MJINI DODOMA

  • Naibu Waziri Katiba na Sheria atembelea Maonesho

 

 Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Geofrey Pinda akipata maelezo kuhusu historia ya miaka 100 ya Mahakama Kuu ya Tanzania kutoka kwa Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi Mhe. David Ngunyale wakati Kiongozi huyo alipotembelea Maonesho ya wiki ya Sheria yanayoendelea mjini Dodoma.

 

Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Geofrey Pinda akiwa kwenye banda la Maonesho la wadau wa Mahakama- Ofisi ya Taifa ya Mashtaka wakati Kiongozi huyo alipotembelea Maonesho ya wiki ya Sheria yanayoendelea mjini Dodoma.
Mkurugenzi wa Idara ya Usimamizi wa Mashauri na Ubora wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali, Aboubakar Mrisha akielezea jambo kwa Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Geofrey Pinda wakati Kiongozi huyo alipotembelea Banda la Ofisi wa Wakili Mkuu wa Serikali katika Maonesho ya wiki ya Sheria yanayoendelea mjini Dodoma.
Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Geofrey Pinda akipata maelezo kuhusu Maboresho ya Huduma za Mahakama kwa upande Ujenzi wa majengo ya Mahakama kutoka kwa Mhandisi wa Mahakama ya Tanzania, Coelestine Rutasindana wakati Kiongozi huyo alipotembelea Maonesho ya wiki ya Sheria yanayoendelea mjini Dodoma.

Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Geofrey Pinda akisaini kitabu cha wageni alipotembelea banda la Mahakama la Kurugenzi ya Menejimenti ya Usimamizi wa Mashauri.



Hakuna maoni:

Chapisha Maoni