Jumatatu, 25 Januari 2021

MATUKIO KATIKA PICHA MAONESHO YA WIKI YA SHERIA

 Zifuatazo ni picha mbalimbali za matukio katika Maonesho ya Maadhimisho ya Wiki ya Sheria na miaka 100 ya Mahakama Kuu ya Tanzania yanayoendelea katika Viwanja vya Nyerere ‘Square’ jijini Dodoma.

Maafisa mbalimbali wa Mahakama pamoja na Wadau wa Mahakama wanaoshiriki katika Maonesho hayo wanaendelea kutoa huduma kwa wananchi wanaotembelea katika Mabanda hayo.

Kamishna Generali wa Uhamiaji Tanzania, Dkt. Anna Peter Makakala (kulia) akizungumza jambo alipotembelea moja ya Mabanda ya Mahakama katika Maonesho ya Wiki ya Sheria na miaka 100 ya Mahakama Kuu ya Tanzanian yanayoendelea katika viwanja vya Nyerere 'Square' jijini Dodoma.

 Muonekano wa sehemu ya mabanda ya Wadau mbalimbali wanaoshiriki katika Maonesho ya Maadhimisho ya Wiki ya Sheria na miaka 100 ya Mahakama Kuu ya Tanzania.

Naibu Msajili, Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma (aliyeketi kulia) pamoja na Maafisa wenzake wa Mahakama wakitoa huduma kwa wananchi waliotembelea katika Maonesho ya Maadhimisho ya Wiki ya Sheria na miaka 100 ya Mahakama Kuu ya Tanzania.
Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Sharmillah Sarwatt (wa pili kushoto) na Maafisa wengine wa Mahakama wakiwa katika picha ya pamoja na Mzee aliyewahi kufanya kazi Mahakama Kuu-Arusha kuanzia mwaka 1968 kama Karani, Mzee Philip Saiguran.
Wananchi wakipata huduma kutoka katika banda la Kurugenzi ya Usimamizi wa Mashauri na Kurugenzi ya TEHAMA-Mahakama ya Tanzania.

Naibu Msajili-Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, Mhe. David Ngunyale akitoa elimu ya sheria kwa wananchi waliotembelea banda la Mahakama Kuu.

Wananchi  wakipata huduma kutoka katika banda la Maboresho na Miundombinu.

 



 

 
 

 

 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni