Na Mary Gwera, Mahakama
Wanachama
wa Chama cha Ushirika cha Akiba na Mikopo cha Mahakama (SACCOS) wametakiwa
kuongeza wigo wa kuutangaza ushirika huo ili watumishi wengine wa Mhimili huo
waweze kujiunga na ushirika huo kwa manufaa mbalimbali.
Akifungua
rasmi Mkutano Mkuu wa mwaka 2020 wa SACCOS-Mahakama mapema leo Januari 16, 2021,
Naibu Msajili wa Mahakama Kuu-Masjala Kuu, Mhe. Nyigulila Mwaseba alisema kuwa Viongozi na Wanachama wa SACCOS waongeze
kasi ya kutangaza faida za Chama hicho.
Mhe.
Mwaseba ambaye alimwakilisha mgeni rasmi Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania,
Mhe. Sharmillah Sarwatt alisema kuwa idadi ya Wanachama wa SACCOS haishabihiani
na idadi iliyopo ya Watumishi wa Mahakama nchini na hivyo kuwashauri kutumia
njia mbalimbali kuongeza idadi yao.
“Kwanza
ninashukuru kwa kuialika Ofisi ya Msajili Mahakama Kuu kuwa mgeni, naomba
nikiri kuwa nimejulishwa faida nyingi za SACCOS ikiwemo kuwasaidia watumishi wa
Mahakama kupata mikopo ya riba nafuu, mikopo kupatikana ndani ya miezi mitatu
ya kuchangia na kadhalika,” alisema.
Aliongeza
kwa kupendekeza kuwa wanachama kutoka kada mbalimbali wawahamasishe ili kupata wanachama
wengine.
Awali
akimkaribisha mgeni rasmi, Mwenyekiti wa SACCOS-Mahakama anayemaliza muda wake,
Bw. Edwin Protas alisema Chama hicho hicho kinakabiliwa na changamoto ya mtaji
mdogo huku akitoa rai kwa watumishi wengine wa Mahakama kujiunga na Chama
hicho.
Katika
mkutano huo ulioshirikisha wanachama kutoka Mahakama mbalimbali nchini,
kutakuwa na uchaguzi mkuu wa Viongozi wa Chama baada ya kumalizika kwa muda wa
viongozi waliokuwepo.
Chama cha Ushirika cha Akiba na Mikopo cha Mahakama (SACCOS) kilianzishwa mnamo mwaka 1970, kwa sasa kina jumla ya Wanachama 335.
Naibu Msajili, Mahakama Kuu-Masjala Kuu, Mhe. Nyigulila Mwaseba akifungua Mkutano Mkuu wa mwaka 2020 wa Chama cha Ushirika cha Akiba na Mikopo cha Mahakama (SACCOS) uliofanyika katika Ukumbi wa Mahakama Kuu-Dar es Salaam.
Mwenyekiti
wa SACCOS-Mahakama, Bw. Edwin Protas akizungumza wakati wa mkutano huo.
Sehemu ya Wanachama wa SACCOS waliohudhuria Mkutano huo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni