Jumatatu, 15 Machi 2021

MTUMISHI WA MAHAKAMA YA MWANZO ZOISSA KONGWA AFARIKI DUNIA

TANZIA
Marehemu Magdalena Thomas Msenga.

Mahakama ya Tanzania inasikitika kutangaza kifo cha Mtumishi wake Bi. MagdalenaThomas Msenga (pichani) kilichotokea usiku wa kuamkia jana Machi 14, 2021.

Marehemu Magreth alikuwa Msaidizi wa Ofisi katika Mahakama ya Mwanzo Zoissa iliyopo Wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma.

Mazishi yanatarajia kufanyika Dar es Salaam Machi 18, 2021.

Mahakama ya Tanzania inaungana na ndugu, jamaa na marafiki katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo ya kuondokewa wa mpendwa wetu.

BWANA AMETOA, BWANA AMETWAA, JINA LAKE LIHIMIDIWE.
Hakuna maoni:

Chapisha Maoni