Jumanne, 30 Machi 2021

TANZIA; MTUMISHI WA MAHAKAMA AFARIKI DUNIA

Marehemu Coelestine Willard Ishengoma

Mahakama ya Tanzania inasikitika kutangaza kifo cha Mtumishi wake, Mhe. Coelestine Willard Ishengoma (pichani), aliyekuwa Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo Ngerengere kilichotokea usiku wa kuamkia Machi 29, 2021.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Mahakama ya Mkoa Morogoro Marehemu Ishengoma alikutwa na umauti katika hospitali ya Taifa Muhimbili alipokuwa akipatiwa matibabu.

Mazishi yanatarajiwa kufanyika Machi 31, 2021 Ngerengere mkoani Morogoro.

Mahakama ya Tanzania inaungana na ndugu, jamaa na marafiki katika kipindi hiki cha majonzi cha kuondokewa na mpendwa wetu.

BWANA AMETOA, BWANA AMETWAA, JINA LAKE LIHIMIDIWE.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni