Mafunzo
elekezi ya siku tatu (3) kwa Wasajili na Watendaji wa Mahakama kuhusu Utunzaji
bora wa kumbukumbu na Nyaraka yaendelea, Mada mbalimbali zatolewa na Wawezeshaji kuimarisha utekelezaji wa majukumu ya Maafisa hao.
Zifuatazo ni picha mbalimbali za matukio ya yanayoendelea kujiri katika Mafunzo hayo yanayofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Mipango jijini Dodoma.
Mhe. Aidan Mwilapwa, Hakimu Mkazi Mkuu kutoka Kurugenzi ya Usimamizi, Ukaguzi na Maadili-Mahakama ya Tanzania akiwasilisha mada kuhusu Usimamizi na Ukaguzi wa Mahakama.
Afisa TEHAMA kutoka Ofisi ya Serikali Mtandao (eGA), Bw. Thomas Malinga akiwasilisha mada ya ofisi mtandao 'e-office' kwa washiriki wa mafunzo hayo. Mahakama ya Mahakama ipo mbioni kuanza matumizi ya ofisi mtandao hali itakayowezesha kupungua matumizi ya karatasi.
Bw. Andrew Msami, mmoja wa Wawezeshaji wa Mafunzo kutoka chuo cha 'ESAMI' akitoa mada ya Uongozi na Utawala mabadiliko 'Leadership and Change Management'.
Washiriki wa mafunzo wakifuatilia mada kwa umakini.
Mkurugenzi wa TEHAMA, Mahakama ya Tanzania, Bw. Kalege Enock akiwasilisha mada ya hali ya matumizi ya TEHAMA kwa upande wa TEHAMA. Aidha, Bw. Kalege aliwakumbusha Washiriki wa Mafunzo baadhi ya mifumo iliyopo Mahakamani ikiwa ni pamoja na Mfumo wa kusajili na kuratibu mashauri kwa njia ya Kielektroniki (JSDS), Mfumo wa Mawakili (TAMS), 'JMAP', TANZLII, MUSE na mifumo mingineyo.
Mkurugenzi wa Usimamizi wa Mashauri, Mahakama ya Tanzania, Mhe. Desdery Kamugisha akiwasilisha mada kuhusu hali ya usimamizi wa mashauri katika Mahakama nchini.
Washiriki wa mafunzo wakifuatilia mada.
Mkurugenzi Msaidizi wa Rasilimali Watu, Bw. Bwai Biseko akiwasilisha mada kuhusu masuala ya mbalimbali ya Kiutumishi, ikiwemo taratibu za utoaji adhabu kwa watumishi wanaokiuka maadili ya Utumishi.
(Picha na Mary Gwera, Mahakama-Dodoma)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni