Jumamosi, 29 Mei 2021

JAJI SIYANI AWAAPISHA MAKAMISHNA WA MAGEREZA KUWA WAJUMBE WA TUME YA UTUMISHI YA JESHI LA POLISI, UHAMIAJI NA MAGEREZA

 Na Stanslaus Makendi- Mahakama Kuu Dodoma

 Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dodoma Mhe. Mustapher Siyani amewaapisha Makamishna wawili wa Jeshi la Magereza kuwa wajumbe wa Tume ya Utumishi ya Jeshi la Polisi, Uhamiaji na Magereza.

Hafla hiyo ya kuapishwa kwa Makamishna hao ilifanyika hivi karibuni  katika Ofisi ya Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma.

Walioapishwa ni Kamishna wa Magereza anayeshughulikia Utawala na Rasilimaliwatu, DCP Jeremiah Yoram Katungu na Kamishina wa Magereza anayeshughulikia masuala ya Sheria, ACP Isack Abel Kangula.

Akizungumza mara baada ya kuwaapisha Makamishna hao, Jaji Siyani aliwasisitiza kushughulikia masuala yote yanayohusu Utumishi wao katika Tume hiyo kwa kuzingatia Sheria zote zinazoongoza Tume husika ili kutenda haki na kuondoa migongano ya kisheria inayohusiana na majukumu wanayoyatekeleza.

Aidha, wajumbe hao wameapishwa kwa mujibu wa kifungu cha 13 (1), (3) cha Sheria ya Tume ya Utumishi ya Jeshi la Polisi, Uhamiaji na Magereza Sura ya 241.

 

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dodoma Mhe. Mustapher Siyani akimuapisha moja wa Makamishna ofisini kwake jijini Dodoma.
Moja wa Makamishna waliapishwa akisaini hati ya kiapo mbele ya Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dodoma Mhe. Mustapher Siyani. Aliyesimama ni Naibu Msajili Mfawidhi wa Kanda hiyo Mhe. Dkt. Angelo Rumisha.

Hafla ya kuapishwa Makamishna ikiendelea. 

 

 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni