Jumapili, 2 Mei 2021

MAHAKAMA KUU KANDA YA MUSOMA YAZINDUA BARAZA LA WAFANYAKAZI

 

Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Mahakama Kuu ya Tanzania kanda ya Musoma wakiimba kwa pamoja wimbo wa Tughe wa Mshikamano Daima wakati wa Mkutano wa Baraza hilo uliofanyika mwishoni mwa wiki mjini Musoma. Kwa mara ya kwanza Baraza hilo limefanyika tangu kuanzishwa kwa Mahakama Kuu kanda ya Musoma.

Baadhi ya Viongozi wa TUGHE wakiwa kwenye Mkutano uliofanyika kwa mara ya kwanda katika Mahakama Kuu Kanda ya Musoma. Wa kwanza kushoto ni Katibu wa TUGHE Mkoa wa Mara Bw. Hamis Mwisa na anayefuata ni Afisa Kazi Mkoa wa Mara Bw. Perfect Kimaty wakifuatilia Mkutano huo.
Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Musoma ambaye pia ni Naibu Msajili wa kanda hiyo Mhe. Eugenia Rujwahuka akisoma hotuba ya Ufunguzi.
 
Mtendaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Musoma, Bw. Festo Chonya akiwasilisha Bajeti pendekezwa ya mwaka wa fedha 2021/2022 katika Baraza hilo.

Baadhi ya washiriki wa Baraza hilo wakisikiliza na kufuatilia kwa makini mada zilizowasilishwa katika Mkutano huo.

Mtumishi wa Mahakama ya Wilaya ya Tarime Bw.Daniel Magussu akichangia jambo katika Mkutano huo wa Baraza.







Hakuna maoni:

Chapisha Maoni