Alhamisi, 8 Julai 2021

WADAU MBALIMBALI WAENDELEA KUTEMBELEA BANDA LA MAHAKAMA NA KUJIPATIA ELIMU





MAHAKAMA NA MATUKIO KATIKA PICHA KWENYE MAONESHO YA 45 YA SABASABA KATIKA VIWANJA VYA MWL. NYERERE JIJINI DAR ES SALAAM 


Baadhi ya wananchi waliojitokeza katika banda la Mahakama ya Tanzania ili kujipatia elimu na machapisho ya Mahakama katika Maonyesho ya 45 ya Sabasaba Jijini Dar es salam


 

Wananchi mwenye ulemavu akitumia ngazi maalumu kuingia kwenye Mahakama inayotembea kwa ajili ya kujifunza jinsi Mahakama hiyo inavyofanya kazi wakati wa Maonesho ya 45 ya Sabasaba Jijini Dar es salaam.


Kiongozi wa Jumuiya ya Waislam Ahmaddiya Tanzania Bw. Tahir Mahmood Chaudhry (wenye kizibao cheusi) akiwa na Viongozi wa Jumuiya hiyo alipotembelea Banda la Mahakama kufahama mambo mbalimbali yanayofanywa na Taasisi hiyo.

Kiongozi wa Jumuiya ya Waislam Ahmaddiya Tanzania Bw. Tahir Mahmood Chaudhry (wenye kizibao cheusi) akiwa na Viongozi wa Jumuiya hiyo alipotembelea Banda la Mahakama kufahama mambo mbalimbali yanayofanywa na Taasisi hiyo wakiwa kwenye picha ya pamoja.


Kiongozi wa Jumuiya ya Waislam Ahmaddiya Tanzania Bw. Tahir Mahmood Chaudhry (wenye kizibao cheusi) akiwa na Viongozi wa Jumuiya hiyo alipotembelea Banda la Mahakama kufahama mambo mbalimbali yanayofanywa na Taasisi hiyo, akisaini kitabu cha wageni alipotembelea kwenye gari maalum la Mahakama Inayotembea.


Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Ardhi Mhe. Salma Maghimbi alipotembelea Banda la Mahakama ya Tanzania kujionea utendaji kazi wa watumishi katika maonesho ya Sabasaba Jijini Dar es salaam.

Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Mwanabaraka Mnyukwa  (mwenye ushungi wa bluu) alipotembelea Banda la Mahakama ya Tanzania kujionea utendaji kazi wa watumishi akipewa ufafanuzi wa jambo katika banda la Mahakama ya Haki ya Afrika Mashariki katika maonesho ya Sabasaba Jijini Dar es salaam.

Wananchi waliojitokeza katika banda la Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Ardhi kujifunza mambo yanayohusu sheria zinazosimamia migogoro ya ardhi.

Wananchi waliojitokeza katika banda la miaka 100 ya Mahakama Kuu ya Tanzania  kujifunza historia ya Mahakama ya Tanzania.

Wananchi waliojitokeza katika banda la Chama cha Wanasheria Tanganika (TLS) wakipewa huduma za Kisheria na Mawakili kutoka Chama hicho.

Baadhi ya wananchi waliotembelea banda la Mahakama kitengo cha Mirathi na Wosia kupata elimu wakati wa maonesho ya 45 ya Biashara Sabasaba.

Naibu Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kituo cha Usuluhishi Mhe. Hamza Wanjah akitoa ufafanuzi wa jambo kwa wananchi waliojitokeza kupata elimu juu ya utatuzi wa migogoro ya ardhi.


Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es salaam Mhe. Joaquine De -Mello akisaini kitabu cha wageni mara alipotembelea Banda la Mahakama ya Tanzania Divisheni ya Biashara.

Picha na Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano - Mahakama.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni