Jumatano, 25 Agosti 2021

WAJUMBE WA KAMATI ZA MAADILI YA MAAFISA WA MAHAKAMA WAJENGEWA UWEZO

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dodoma, Mhe. Mustapher Siyani amefungua mafunzo ya kuzijengea uwezo Kamati za Maadili ya Maafisa wa Mahakama ili waweze kutekeleza vema jukumu lao la usimamizi wa maadili ya Maafisa hao kwenye maeneo yao ya kiutawala.

Akifungua mafunzo hayo yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa mikutano wa Mkuu wa Mkoa Dodoma Jana Agosti 24,2021, Jaji Siyani aliwakumbusha wajumbe umuhimu wa kamati hizo kufanya vikao hivyo, kwani zimeundwa kwa mujibu wa sheria, ni vema kutumia vikao hivyo kuchunguza mienendo ya Maafisa hao katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku.

Kwa upande wa Wajumbe, nao wameishukuru na kuipongeza Tume ya Utumishi wa Mahakama ya Tanzania kwa kuwapatia mafunzo hayo yaliyowapa uelewa na kuweza kutambua nafasi zao kiutendaji na kushauri mafunzo hayo kuwa endelevu.

Aidha, Wajumbe wameishauri Tume ya Utumishi wa Mahakama kuangalia uwezekano wa kuwapatia wajumbe wa Kamati hizo kanuni za maadili ya Maafisa wa Mahakama na ikiwezekana nakala hizo ziwe zile zilizotafsiriwa kwa lugha ya Kiswahili 

Kikao hicho kimejumuisha wajumbe wa Kamati za Maadili ya Maafisa wa Mahakama za Mkoa wa Dodoma pamoja na wilaya zake wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa na Wakuu wa Wilaya zote za Mkoa huo.

Tume hiyo itaendelea kutoa mafunzo ya aina hiyo kwa Mikoa ya Singida, Shinyanga na kuhitimisha awamu hiyo na Mkoa wa Simiyu. 

Wajumbe wa Kamati za Maadili ya Maafisa wa Mahakama wakiwa kwenye Ukumbi wa mikutano wa Mkuu wa Mkoa Dodoma Jana Agosti 24,2021, wakijengewa uwezo ili waweze kutekeleza vema jukumu lao la usimamizi wa maadili ya Maafisa hao kwenye maeneo yao ya kiutawala.

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dodoma, Mhe. Mustapher Siyani akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Anthony Mtaka wakati wa mafunzo hayo yaliyofanyika Jijini Dodoma.

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Temeke, Mhe. Ilvin Mugeta akitao mada wakati wa mafunzo hayo ya kuwajengea uwezo wajumbe wa kamati za Maadili za Maafisa wa Mahakama yaliyofanyika mkoani Dodoma.
Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mhe.Remidius Emmanuel akichangia mada wakati wa mafunzo hayo ya kuwajengea uwezo wajumbe wa kamati za Maadili za Maafisa wa Mahakama yaliyofanyika mkoani Dodoma.

Baadhi ya Wajumbe wa Kamati za Maadili ya Maafisa wa Mahakama wakifuatilia mafunzo hayo.

Baadhi ya Wajumbe wa Kamati za Maadili ya Maafisa wa Mahakama wakifuatilia mafunzo hayo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni