Wadau wa Haki Jinai na Madai wamekutana na kufanya kikao cha kupitia Mwongozo wa uendeshaji wa Vituo Jumuishi vya Utoaji Haki kilichofanyika leo Agosti 24, 2021 katika Ukumbi wa Karimjee Jijini Dar es salaam.
Kikao hicho kililenga kutoa elimu kwa wadau wa Mahakama juu ya kuanzishwa kwa huduma hizo pamoja na kutekeleza nguzo ya tatu ya Mpango Mkakati wa miaka mitano wa Mahakama ya Tanzania inayohusu kurejesha imani ya wananchi kwa Mhimili wa Mahakama na ushirikishwaji wa wadau.
Mara baada ya kikao wadau hao walipata wasaa wa kutembelea Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki (One Stop Center) maalum kwa ajili ya kusikiliza mashauri yanayohusu Mirathi, Ndoa, Talaka na Watoto kilichojengwa katika Manispaa ya Temeke Jijini Dar es salaam. Kituo hki kiko katika hatua za mwisho za ujenzi na kinatarajiwa kuanza kufanya kazi ifikapi Oktaba mwaka huu.
Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Prof. Elisante Ole Gabriel (aliyesimama) akifungua mkutano wa Wadau wa Haki Jinai na Madai (hawapo pichani) wa kupitia Mwongozo wa uendeshaji wa Vituo Jumuishi vya Utoaji Haki, uliofanyika katika Ukumbi wa Karimjee Jijini Dar es salaam, leo Agosti 24,2021, wengine Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Morogoro Mhe. Paul Ngwembe (kulia) na Msajili Mkuu wa Mahakama Mhe. Wilbert Chuma (kushoto).
Wadau wa Haki Jinai na Madai wakiwa kwenye picha ya pamoja na Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Prof. Elisante Ole Gabriel (wa Tatu kulia mbele) mara baada ya kupitishwa kwenye Mwongozo wa uendeshaji wa Vituo Jumuishi vya Utoaji Haki vinavyotarajiwa kuanza kutoa huduma mara baada ya kukamilika kwake, wengine ni Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Morogoro Mhe. Paul Ngwembe (katikati), Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania na Mkuu wa Kitengo cha Maboresho ya Mahakama, Mhe Zahra Maruma( wa pili kushoto), Mkurugenzi wa Mashtaka Mhe. Sylvester Mwakitalu (wa tatu kushoto), Msajili Mkuu wa Mahakama Mhe. Wilbert Chuma (wa pili Kulia), Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Sharmillah Sarwatt (wa kwanza kushoto) na Mwakilishi kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Bw. Shilogile (wa kwanza kulia).
Wadau wa Haki Jinai na Madai wakiwa pamoja mbele ya jengo la Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki walipokimbelea ili kujionea maendeleo ya ujenzi wa Kituo hicho kinachojengwa Manispaa ya Temeke Jijini Dar es salaam.
Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Prof. Elisante Ole Gabriel (aliyenyoosha mkono) akielekeza jambo alipotembelea Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki cha Manispaa ya Temeke akiwa na wadau kukagua maendeleo ya ujenzi wa Kituo hicho.
Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Prof. Elisante Ole Gabriel (aliyechuchumaa) akikagua njia za mifumo ya TEHAMA akisaidiwa na Mkuu wa Kitengo cha Usimamizi wa Majengo wa Mahakama Mhandisi Khamadu Kitunzi kwenye jengo la Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki linaloendelea kujengwa katika Manispaa ya Temeke Jijini Dar es salaam. Jengo hilo linatarajiwa kukamilika karibuni.
Mkuu wa kitengo cha Usimamizi wa Majengo wa Mahakama ya Tanzania Mhandisi Khamadu Kitunzi, akiwaongoza na kutoa maelezo kwa wadau waliotembelea Kituo Jumuishi cha utoaji haki kinachojengwa Manispaa ya Temeke Jijijni Dar es salaam walipokitembelea kujionea maendeleo yake.
Mmoja ya wadau wa kikao hicho cha Mwongozo wa Uendeshaji wa Vituo Jumuishi vya utoaji haki akichangia mada.
Baadhi ya Wadau waliohudhuria kikao cha Mwongozo wa Uendeshaji wa Vituo Jumuishi vya utoaji haki
Baadhi ya Wadau waliohudhuria kikao cha Mwongozo wa Uendeshaji wa Vituo Jumuishi vya utoaji haki.
(Picha na Innocent Kansha - Mahakama)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni