Jaji Ruhumbika enzi ya Uhai wake, akiapishwa na Rais wa Awamu ya Kwanza Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania
Jaji Mstaafu wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Raymond John Lwegongwa Ruhumbika amefariki dunia jana Agosti 23, 2021 katika hospitali ya mkoa wa Dodoma.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Uongozi wa
Mahakama, taarifa zaidi kuhusiana na msiba wa Jaji Mstaafu Ruhumbika zitapatikana
hapo baadaye.
Marehemu Jaji Ruhumbika alizaliwa Machi 17 mwaka
1933 mkoani Mwanza. Aliajiriwa na Mahakama ya Tanzania April 1, mwaka
1964. Aidha, Juni 29 mwaka 1981 aliteuliwa na Rais wa awamu ya
Kwanza Mwalimu Julius Nyerere kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania.
Alikitumikia cheo hicho mpaka Machi 17 mwaka 1993 alipostaafu kwa mujibu
wa sheria.
Mahakama ya Tanzania inatoa pole kwa ndugu, jamaa, marafiki
pamoja na watumishi wote wa Mahakama kufuatia msiba huo.
BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA, JINA LAKE LIHIMIDIWE
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni