Jumapili, 7 Novemba 2021

JAJI MKUU PROF.JUMA AZURU KABURI LA BABA WA TAIFA

 Jaji Mkuu wa Tanzania,  Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akitoa heshima katika kaburi la Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Hivi karibuni akiwa katika ziara yake ya kikazi Kanda ya Musoma, Mhe. Prof. Juma alipata nafasi ya kutembelea nyumbani kwa Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere katika kijiji cha Butiama ambapo alitumia nafasi hiyo kutoa heshima katika kaburi la Hayati Mwalimu Nyerere.


Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akiweka shada la maua katika kaburi la Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere wakati alipotembelea nyumbani kwa Baba wa Taifa hivi karibuni.

Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma (kushoto) akipolelewa na Madaraka Nyerere pamoja na wanafamilia wengine alipowasili nyumbani kwa Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. 


Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akiangalia maktaba iliyosheheni vitabu mbalimbali aliyokuwa akiitumia Hayati Mwalimu Nyerere wakati wa uhai wake.

Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akiangalia sanamu ya kuchonga ya chuma ya Mwalimu Nyerere,  huku akipata maelezo kutoka kwa mwanafamilia, Bi. Gaudencia Waziri.

  •  

 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni