Alhamisi, 25 Novemba 2021

JAJI MWAIKUGILE AZIKWA

Na Margreth Kinabo, Mahakama.

Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma jana tarehe 24 Novemba, 2021 ameongoza mamia ya watumishi wa Mahakama ya Tanzania na wananchi wengine kuuaga mwili wa Jaji Mstaafu wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Njengafibili Mwaikugile aliyefariki dunia tarehe 20 Novemba, 2021 jijini Dar es Salaam.

Shughuli za kuaga mwili wa marehemu Mwaikugile zilifanyika nyumbani kwake Sala Sala Juu Wilaya ya Kinondoni Mkoa wa Dar es Salaam ambapo viongozi mbalimbali wa Mahakama na Majaji wastaafu walishiriki. Viongozi wengine wa Mahakama waliohudhuria maziko hayo ni Jaji Kiongozi, Mhe. Mustapher Siyani, Msajili Mkuu, Mhe. Wilbert Chuma, Mtendaji Mkuu, Prof. Elisante Ole Gabriel na baadhi ya Majaji wastaafu, akiwemo Jaji Mkuu mstaafu Barnabas Samatta.

Baada ya heshima za mwisho kutolewa nyumbani kwake, mwili wa marahemu ulipelekwa katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) kwa ajili ya ibada kabla ya kupumzishwa kwenye nyumba yake ya milele.

Marehemu Mwaikugile alianza kuhudumu katika Mahakama ya Tanzania tangu 1982 kama Hakimu na baadaye kupanda katika ngazi mbalimbali za utumishi kama Msajili wa Mahakama Kuu na baadaye Mahakama ya Rufani kabla ya kuteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu tarehe 28 Februari, 2003, nafasi ambayo ameitumikia hadi alipostaafu tarehe 15 Oktoba, 20214.

Mwili wa Jaji Mstaafu wa Mahakama Kuu ya Tanzania, marehemu Njengafibili Mponjoli Mwaikugile ukiingizwa katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) jana, lililopoMtaa wa Salasala Juu, Jijini Dar es Salaam.


Mwili wa Jaji Mstaafu wa Mahakama Kuu ya Tanzania, marehemu Njengafibili Mponjoli Mwaikugile ukiwa ndani ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT). 

Mke wa marehemu Jaji Mstaafu wa Mahakama Kuu ya Tanzania, marehemu Njengafibili Mponjoli Mwaikugile, Bi. May Kivugo (wa pili kushoto mwenye gauni la pinki) akiwa pamoja na watoto walioko msatari wa mbele, wakati wa ibada hiyo wengine ni ndugu na jamaa na marafiki.

Wanakwaya wakiwa katika ibada kumwombea Marahemu Mwaikugile. 

Sehemu ya waombolezaji wakiwa katika ibada kumwombea Marahemu Mwaikugile. 

Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma(katikati) akiwa katika ibada hiyo, (kushoto wa kwanza) ni Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Mustapher Siyani, wa (pili kushoto) ni Jaji Mkuu Mstaafu wa Tanzania, Mhe. Barnabas Samatta. Wengine kulia wa pili ni Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania, Mhe. Mussa Kipenka na wa kwanza kulia ni Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Tanzania, Mhe. John Mrosso.

Mtoto wa marehemu akisoma wasifu wa marehemu baba yake.

Mkuu wa Jimbo la Kaskazini Mchungaji Jacob Mwangomola akielezea jinsi marehemu alivyokuwa mcha mungu hadi kutoa sehemu ya kiwanja chake kwa ajili ya ujenzi wa kanisa hilo.

Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Wilbert Chuma akizungumza jambo.

Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Mustapher Siyani, akielezea jinsi marehemu Jaji Mwaikugile alivyokuwa akiishi na watu kwamba hakuwa mchoyo wa ujuzi na hakuwa mbaguzi.

Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akitoa heshima za mwisho kwa Jaji Mstaafu wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Marehemu Njengafibili Mponjoli Mwaikugile.

Jaji Mkuu Mstaafu wa Tanzania, Mhe. Barnabas Samatta akitoa heshima za mwisho Jaji Mstaafu wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Marehemu Njengafibili Mponjoli Mwaikugile.

Majaji Wastaafu wa Mahakama ya Rufani Tanzania wakitoa heshima za mwisho Kulia ni Jaji John Mrosso na kushoto Jaji Mussa Kipenka.

Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Mhe. Mustapher Siyani akitoa heshima za mwisho Jaji Mstaafu wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Marehemu Njengafibili Mponjoli Mwaikugile.

Jaji Mstaafu wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Sophia Wambura (aliyebana nywele) akitoa heshima za mwisho.

Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Wilbert Chuma akitoa heshima za mwisho.

Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Prof. Elisante Ole Gabriel akitoa heshima za mwisho. 


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni