Na Innocent Kansha - Mahakama
Mtendaji Mkuu wa Mahakama
ya Tanzania, Prof. Elisante Ole Gabriel leo tarehe 22, Desemba 2021, amekutana na
kufanya mazungumzo na Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Prof.
Edward Hosea ambapo wamekubaliana kuendelea kufanya kazi kwa ukaribu kwa
manufaa ya Taasisi hizo.
Akizungumza na Prof.
Hosea ofisini kwake Jijini Dar es salaam, Mtendaji Mkuu wa Mahakama amemhakikishia
kuendeleza ushirikiano uliopo miongoni mwa Taasisi hizo ili kuondoa kero na migogoro
isiyo ya lazima kwa maslahi ya Taifa.
“Tutaendelea
kubadilishana uzoefu mara kwa mara tutakapopata nafasi ya kufanya hivyo ili
kutatua changamoto zitakazojitokeza kwenye utendaji kazi ikiwemo kupeana
taarifa, hasa za matumizi ya mifumo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) katika kuboresha utendaji na mawasiliano”,
alisema Prof. Ole Gabriel.
Kwa upande wake Rais wa
TLS alimshukuru Prof. Ole Gabriel na kumhakikishia kuendeleza ushirikiano uliopo
baina yao ili kuhakikisha wananchi wanatatuliwa kero zao kupitia Mhimili wa Mahakama.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni