Na. Francisca Swai – Mahakama, Musoma
Jaji
Mfawidhi wa Mahakama ya Tanzania, Kanda ya Musoma, Mhe. Fahamu Mtulya
amesisitiza utambuzi wa mipaka ya maeneo ya Mahakama zote ili kulinda maeneo hayo
dhidi ya uvamizi wa wananchi na taasisi mbalimbali.
Mhe.
Mtulya ametoa kauli hiyo jana tarehe 23 Machi, 2022 akiwa katika siku ya tano
ya ziara yake ya ukaguzi wa shughuli za Mahakama katika Kanda ya Musoma.
Alisema
historia ya maeneo na mipaka ya Mahakama ipo kwa watumishi wa zamani, kiasi
ambacho wasipokuwepo Mahakama inaweza kupoteza utambuzi wa maeneo hayo, jambo
litakalopelekea kupoteza sehemu kubwa ya ardhi yenye thamani.
Aidha,
Jaji Mfawidhi huyo alimtembelea Mkuu wa Wilaya ya Rorya, Mhe. Juma Chikoka
ambapo, pamoja na mambo mengine alitoa rai kwa Mtendaji wa Mahakama, Kanda ya
Musoma , Bw. Festo Chonya kushirikiana na viongozi wa Wilaya ili kupata hati
miliki za kiserikali mapema za maeneo yote ya Mahakama.
Mhe.
Mtulya pia alietembelea na kukagua Mahakama ya Mwanzo Kinesi iliyoanza kutoa huduma Agosti 1, 2020 baada ya Mtendaji wa Mahakama Kanda ya Musoma kufanya
ukarabati wa jengo moja lililokuwa chakavu kutokana na uhitaji wa Mahakama eneo
hilo. Mahakama hiyo ilifungwa mwaka 2000 kutokana na uchakavu wa majengo.
Naye
Mtendaji wa Mahakama Kanda ya Musoma alieleza kuwa kwa sasa kuna mradi
unaoendelea wa ujenzi wa jengo jipya la kisasa la Mahakama hiyo unaotekelezwa
na Mkandarasi PEK Brothers. Mradi huo ni wa miezi nane na ulianza Februari 24,
2022, hivyo unatarajiwa kukamilika Oktoba 23, 2022.
Hakimu
Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Mwanzo Riagoro, Mhe. Boniphace Shimbe akimuonesha
Jaji Mfawidhi wa Mahakama ya Tanzania, Kanda ya Musoma, Mhe. Fahamu Mtulya na
viongozi wengine eneo na mipaka ya Mahakama ya Mwanzo Riagoro.
Jaji
Mfawidhi wa Mahakama ya Tanzania, Kanda ya Musoma, Mhe. Fahamu Mtulya (wa pili
kulia mstari wa mbele) akiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Wilaya Rorya,
Mhe. Juma Chikoka (katikati) pamoja na viongozi wengine wa kamati ya ulinzi na
usalama wa Wwilaya ya Rorya.
Watumishi
wa Mahakama ya Mwanzo Kinesi wakipokea kwa furaha vitendea kazi kutoka kwa Jaji
Mfawidhi wa Mahakama ya Tanzania, Kanda ya Musoma, Mhe. Fahamu Mtulya (katikati).
Kulia ni Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Mwanzo Kinesi, Mhe. Deodath Ngowi
na kushoto ni Mlinzi wa Mahakama hiyo, Bw. Edwin Elisamehe.
Watumishi
wa Mahakama ya Mwanzo Riagoro wakipokea vitendea kazi kutoka kwa Jaji Mfawidhi
wa Mahakama ya Tanzania, Kanda ya Musoma, Mhe. Fahamu Mtulya.
Jaji
Mfawidhi wa Mahakama ya Tanzania, Kanda ya Musoma, Mhe. Fahamu Mtulya (wa pili
kulia) akimkabidhi vitendea kazi watumishi
wa Mahakama ya Mwanzo Riagoro akiwemo Hakimu Mkazi Mfawidhi Mhe. Ole Shady
Marwa (pili kushoto).
Hakimu
Mkazi Mfawidhi Mahakama ya Mwanzo Shirati, Mhe. Simon Msangazi akimuonesha Jaji
Mfawidhi wa Mahakama ya Tanzania, Kanda ya Musoma, Mhe. Fahamu Mtulya na
viongozi wengine maeneo ya Mahakama hiyo.
Jaji
Mfawidhi wa Mahakama ya Tanzania, Kanda ya Musoma, Mhe. Fahamu Mtulya akitoa
maelekezo kwa watumishi wa Mahakama ya Mwanzo Kinesi.
Watumishi
wa Mahakama ya Mwanzo Shirati wakisikiliza kwa makini maelekezo ya Jaji
Mfawidhi wa Mahakama ya Tanzania, Kanda ya Musoma, Mhe. Fahamu Mtulya (kushoto).
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni