Na Innocent Kansha – Mahakama, Dododma
Jaji Mfawidhi
wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dodoma, Mhe. Gerson Mdemu ametoa wito kwa
Wahasibu na Wakaguzi wa Ndani kutumia mafunzo watakayopata kuhakikisha yanatekeleza
dira ya Mahakama na kusaidia kutatua kero za wadaawa ili huduma zitolewe kwa
haraka, weledi, wepesi na ufanisi wa hali ya juu.
Akifungua
mafunzo ya kundi la pili la Wahasibu na Wakaguzi wa Ndani ya siku tano katika
Ukumbu wa Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki Jijini Dodoma leo tarehe 6 Juni, 2022, Jaji Mdemu alisema dira ya Mahakama haiwezi kutekelezeka iwapo mifumo ya kihasibu
watakayojifunza haitosaidia kuondoa usumbufu kwa wadaawa wakati wa kufanya
malipo mbalimbali ya usajili wa mashauri na nyaraka za kimahakama, kulipa
mirathi kwa wakati na watumishi wa ndani kupata stahiki zao bila usumbufu na
kucheleweshwa.
“Pengine jambo
la msingi ambalo mnatakiwa kulifahamu na kupitia mafunzo haya mtalifahamu ni
kuwa dira ya upatikanaji
wa haki kwa wakati na kwa wote haitafanikiwa kwa dhana kwamba inawahusu maafisa wa
Mahakama tu, bali hata ninyi pia mna nafasi kubwa ya kuhakikisha matamanio ya taasisi yanafikiwa katika utoaji wa huduma ya haki unaomlenga mteja na hivyo
mtakwenda kutenda kwa vitendo”, aliongeza Jaji Mdemu.
Mhe. Mdemu
akatoa rai kwa Wahasibu na Wakaguzi wa Ndani kutumia ujuzi na taarifa za msingi
watakazobadilisha kupitia wakufunzi katika mafunzo hayo kuhusu matumizi bora ya
Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) kutatua changamoto za utoaji wa
huduma za kihasibu ili kurahisisha na kuondoa usumbufu kwa wadaawa watakao wahudumia.
Alisema kuwa TEHAMA ndiyo
msingi wa dira ya kurahisisha upatikanaji wa huduma, kwa kuwa washiriki hao wa mafunzo ndiyo watakaofunzwa
kuhusu matumizi ya hiyo mifumo, hivyo wanapaswa kutokuwa kikwazo cha utoaji huduma bora
kwa wadaawa.
“Mahakama ya
Tanzania inanuwia kuwa na maamuzi bora ya kimahakama ambapo imejiwekea malengo
ya kukuza uelewa wa misingi ya taaluma ya kisheria na kuongeza ujuzi kwa
watumishi wa Mahakama. Katika kutekeleza malengo hayo, Mahakama
imejiwekea mkakati wa kuwajengea uwezo watumishi wa ngazi zote. Mmejengewa
uwezo kwenye eneo lenu la kihasibu. Sasa hakutakuwa na kisingizio cha
kuchelewesha huduma, hususani masuala ya mirathi ambayo yanahitimisha maamuzi
yanayotolewa na Mahakimu na Majaji”, aliongeza Jaji Mfawidhi
Jaji
Mdemu akasema ratiba ya mafunzo yatahusu maeneo ambayo yameainishwa
kama vile Mpango Mkakati wa Mahakama (Judiciary Strategic Plan), Njia sahihi ya
kushughulikia mfumo wa masurufu (Appropriate Configuration of System Imprest Management),
Jinsi ya kulipa malipo ya kabla kwenye mfumo pamoja na mzunguko wake (Recording
of System Ledgers for Prepayment Transactions,
Suspense Accounts and Clearing Accounts), Jinsi gani akaunti za kuhamisha fedha
zinavyofanya kazi (Overview of GePG Payment Systems; Proper MUSE functions),
Jinsi gani mfumo wa kielektroniki wa mapato serikalini unatoa huduma (Roles and
Responsibilities of Accounts in Accounting Electronics and Technological
systems),
Maeneo
mengine ya mafunzo hayo yatahusu Jinsi gani mfumo wa malipo serikalini
unavyofanya kazi (Ageing analysis for Debtors and Creditors in Accounting
Systems; Previewing of Accounts (ledger Accounts), Mkataba wa huduma kwa mteja (Client
Service Charter), Huduma kwa mteja na maadili (Customer Service and Ethics
Issues) Professionalism in Accounts and Code of good conduct, Introduction to various GePG reports and their uses, Periodic GePG Reconciliation;
Psychological Issues.
Jaji Mdemu alisema maeneo yote yatakayofundishwa na wawezeshaji ni muhimu na yanahusu utekelezaji wa majukumu yao kama Wahasibu na Wakaguzi wa Ndani kitaaluma na kimaadili. “Mtapewa nyenzo muhimu za utekelezaji kwenye maeneo mengine yaliyo nje ya taaluma yenu lakini hayaepukiki katika kuhakikisha mnatimiza wajibu wenu kutoa huduma ya kihasibu. Mlikuwa na mtakuwa na majadiliano mbalimbali ambayo yatawawezesha kubadilishana uzoefu katika kazi zenu, mkayatumie yote mtakayoyapata katika kufanyia kazi”, alisema Jaji Mdemu.
Mafunzo haya ni sehemu ya utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Mahakama 2020/2021-2024/2025 ambapo katika Tunu ya Tano kuhusu weledi, Mahakama itatekeleza majukumu ya utoaji haki kwa umahiri na ufanisi. Aidha, ndani ya Mpango Mkakati huo, katika nguzo ya kwanza inayohusu utawala, uwajibikaji na usimamizi wa rasilimali, moja ya lengo ni kuwajengea uwezo watumishi wa ngazi zote.
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dodoma, Mhe. Gerson Mdemu (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na washiriki wa mafunzo wa kada ya Wahasibu, wengine ni Naibu Msajili Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dodoma Mhe. Bernard Mpepo (wa pili kulia) na kushoto ni Mtendaji wa Mahakama Kuu, Kanda ya Dodoma Bw. Sumera Manoti (wa pili kushoto) ni Mkurugenzi Msaidizi wa Kitengo cha Mafunzo Mahakama ya Tanzania, Bi. Patricia Ngungulu (wa pili kushoto) na Muhasibu Mwandamizi Mwandamizi Mahakama ya Tanzania Bw. Venant Kambuga (wa kwanza kulia).
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni