Na Festo Sanga-Mahakama, Kigoma
Mahakama
Kuu ya Tanzania, Kanda ya Kigoma, kwa kushirikiana na Mamlaka za Serikali za
Mitaa imeanza kutekeleza kwa vitendo agizo la Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof.
Ibrahim Hamis Juma alilolitoa hivi karibuni alipokuwa katika ziara ya Mahakama,
Kanda ya Tanga, la kutambua na kuweka vibao vya anwani za makazi katika majengo
ya Mahakama.
Hayo
yalibainishwa na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Kigoma, Mhe. Lameck Mlacha wakati wa hafla fupi ya
uzinduzi wa zoezi la kuweka anuani za makazi katika majengo ya mahakama lililofanyika
katika jengo la Mahakama Kuu Kigoma tarehe 31 Mei 2022.
Katika
hafla hiyo, Mhe. Mlacha alisema kuwa zoezi hilo litazifanya Mahakama zilizopo katika
Kanda yake kutambulika kwa urahisi na wateja, hivyo kuwezesha utoaji wa huduma za
hai kwa wakati.
Naye
Mtendaji wa Mahakama katika Kanda ya Kigoma, Bw. Moses Mashaka alieleza kuwa pamoja
na kutekeleza zoezi la anwani za makazi kila Mahakama imeanza utekelezaji wa
kutumia anwani mpya kwenye barua za kiofisi.
Hata
hivyo alieleza kuwa zoezi la utambuzi na uwekaji wa vibao vya namba na anwani
halijakamilika kwenye Mahakama za Mwanzo nane zisizofanya kazi kutokana na
uchakavu mkubwa wa majengo hayo kiasi cha kutotambuliwa na watendaji wa Mamlaka
za Serikali za Mitaa na Mahakama 2 zinazofanya kazi kwa kutumia majengo ya maafisa
Tarafa ambazo ni Manyovu na Kasangezi. Alizitaja
Mahakama hizo za Mwanzo ambazo hazifanyi kazi kama Nyavyumbu, Mgunzu, Kumsenga,
Buhoro, Mnyegera, Mwayaya, Mgambo na Kagunga.
Alibainisha
kuwa jitihada zinafanywa kwa kushirikiana na Mamlaka husika kuzitambua Mahakama
hizo, kupata namba za majengo, jina la barabara au mtaa na postikodi kwa
urahisi wa uandaaji wa anwani za maeneo hayo ili kukamilisha zoezi kwa asilimia
mia moja.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni